Pata taarifa kuu
INDIA

Mwanahabari nguli India auawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake

Mwandishi wa habari nguli nchini India ambaye pia alikuwa mkosoaji mkubwa wa chama cha siasa chenye msimamo mkali cha Hindu ameuawa kwa kupigwa kusini mwa jimbo la Karnataka, polisi nchinik India wamethibitisha.

Polisi wa India wakiweka ulinzi nje ya nyumba ya mwanahabari Gauri Lankesh aliyeuawa usiku wa kuamkia leo. September 6, 2017
Polisi wa India wakiweka ulinzi nje ya nyumba ya mwanahabari Gauri Lankesh aliyeuawa usiku wa kuamkia leo. September 6, 2017 REUTERS/Nivedita Bhattacharjee
Matangazo ya kibiashara

Gauri Lankesh alikutwa ameuawa nje ya mlango wa kuingia nyumbani kwake kwenye mji wa Bangalore.

Polisi wanasema mwanahabari huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na kifuano na watu waliokuwa kwenye pikipiki. Mpaka sasa haijafahamika sababu za kuuawa kwake na uchunguzi tayari umeanza.

Lankesh ni mmoja wa waandishi wa habari maarufu kuuawa nchini India katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti zinazotolewa na wanaharakati nchini India, zinasema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakilengwa na wanasiasa wa chama cha Hindu chenye msimamo mkali.

Katika miaka ya hivi karibuni waandishi wa habari ambao wamekuwa wakosoaji wa chama cha kitaifa cha Hindu wamekuwa wakishambuliwa kwenye mitandao ya kijamii na wakati mwingine kutishiwa kuuawa hata kubakwa.

Mawaziri pia kutoka chama tawala cha Bharatiya Janata BJP na wenyewe waziwazi wamekuwa wakosoaji wakubwa kwa waandishi wa habari wakiwapa majina ya waandishi wa habari wanaojiuza.

Gauri Lankesh alikuwa akifahamika kama Gauri na alikuwa mhariri wa gazeti la kila wiki na alijulikana pia kwa kuwa jasiri na asiyeogopa kukosoa.

Alifahamika pia kwa kuwa mkosoaji mkubwa wa chama cha Hindu chenye msimamo mkali pamoja na kile chama tawala cha BJP.

Amefanya kazi pia na gazeti ya The Times of India.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.