Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JAPAN-USALAMA

Korea Kaskazini yaionya Japan

Nchi ya Korea Kaskazini imeionya Japan kuwa itaharibikiwa kwa kuamua kuchukua upande wa serikali ya Marekani kauli inayotoa siku chache tu baada ya kurusha kombora lililovuka ardhi ya Japan.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ainonya Japan kutoendelea kuiunga mkono Marekani katika maamuzi yake.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ainonya Japan kutoendelea kuiunga mkono Marekani katika maamuzi yake. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani jaribio hilo na kutaka umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi dhidi ya Korea kaskazini.

Katika hatua nyingine mkutano wa kimataifa wa kupinga matumizi ya silaha kali umeendelea jijini New York huku wajumbe wake nao wakilaani jaribio la Korea Kaskazini.

Balozi wa Uingereza kwenye mkutano huo Robert Wood amesema Korea Kaskazini ni tishio kwa usalama wa dunia.

Wakati huo huo Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov ameionya Marekani kuyapa kipaumbele mazungumzo kuliko kuiweka vikwazo zaidi Korea Kaskazini.

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amemueleza Waziri wa Ulinzi wa Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini ni kama kumwagia maji kwenye mgongo wa bata.

Hata hivyo Bw. Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Siku moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani jaribio la Korea Kaskazini Siku ya Jumatano, rais wa Marekani Donald Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo na Korea Kaskazini sio suluhisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.