Pata taarifa kuu
URUSI

Shambulizi lasababisha vifo vya watu 10 katika kituo cha garimoshi nchini Urusi

Watu 10 wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kutokea kwa shambulizi katika kituo cha kupanda garimoshi mjini St. Petersburg, nchini Urusi.

Shambulizi katika kituo cha garimoshi mjini Petersburg nchini Urusi April 3 2017
Shambulizi katika kituo cha garimoshi mjini Petersburg nchini Urusi April 3 2017 Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea katika kituo maarufu cha Sennaya Ploshchad, na waliothirika ni wale waliokuwa ndani ya garimoshi hilo.

Idadi ya watu waliojeruhiwa haijafahamika lakini abiria wengi wameonekana wakililia maumivu  huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.

Picha katika mitandao ya kijamii zinaonesha namna gari moshi hilo lilivyoharibika kwa ndani na milango kurushwa mbali.

Vyombo vya Habari nchini Urusi vinaripoti kuwa rais Vladimir Putin alikuwa katika mji huo wakati shambulizi hili lilipotokea na tayari amepata habari kuhusu kilichojiri.

Hadi sasa haijafahamika waliohusika na shambulizi hili.

Vituo vingine vya magarimoshi katika mji huo yamefungwa kutokana na shambulizi hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.