Pata taarifa kuu
URUSI

Mahakama Urusi yamuhukumu kifungo cha miezi 15 jela kinara wa upinzani

Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amefungwa jela kwa siku 15 baada ya kupatikana na kosa la kukataa kutii maagizo ya polisi wakati wa maandamano dhidi ya serikali mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi  Alexei Navalny akiwa Mahakamani akisikiliza kesi dhidi yake kabla ya kufungwa jela Machi 27 2017
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny akiwa Mahakamani akisikiliza kesi dhidi yake kabla ya kufungwa jela Machi 27 2017 REUTERS/Tatyana Makeyeva
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na kifungo hicho, Navalny ametakiwa kulipa faini ya Dola za Marekani 350 kwa kupanga na kushiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku.

Utawala wa Urusi umekashifu maandamano hayo ya kupinga vitendo vya rushwa dhidi ya serikali, ukisema maandamano hayo ni ya “uchokozi” na kuongeza kuwa vijana wadogo walipewa hela kuandamana.

“Tulichoshuhudia mwishoni mwa juma kwenye maeneo kadhaa hasa Moscow ni uchokozi na uongo,” amesema msemaji wa Serikali ya Moscow Dmitry Peskov.

Mpaka sasa zaidi ya waandamanaji 1000 wamekamatwa na polisi kutokana na kushiriki kwao kwenye maandamano hayo.

Serikali inasema vijana wengi walilipwa fedha ili washiriki kwenye maandamano hayo na kwamba watazawadiwa ikiwa wangekamatwa na vyombo vya usalama nchini humo.

Hata hivyo Peskov alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu chanzo cha habari ya vijana kulipwa fedha, alishindwa kuweka wazi na badala yake akashikilia msimamo kuwa Serikali inayotaarufa kuwa vijana walioshiriki kwenye maandamano haya walilipwa.

Maelfu ya watu waliandamana kwenye mji wa Moscow na maeneo ya miji mingine nchini Urusi siku ya Jumapili, katika maandamano yaliyoandaliwa na Navilny, mwanasheria na mkosoaji mkubwa wa utawala wa rais Vladmir Putin.

Navalny aliwataka wafuasi wake kuandamana siku ya Jumapili, baadaya timu yake kuchapisha ripoti inayodai kuonesha kuwa waziri mkuu Dmitry Medvedev ana miliki baadhi ya majengo na biashara lukuki nchini humo.

Maelfu ya raia walikamatwa kwenye miji mbalimbali nchini humo baada ya mamlaka kwenye miji kingine kukataa kutoa kibali cha kufanyika kwa maandamano hayo.

Katika hatua nyingine Alexei Navalny tayari amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya mjini Moscow, akikabiliwa na mashtaka ya kuandaa maandamano yaliyopigwa marufuku.

Kiongozi huyu pia amezuiliwa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya rushwa, tuhuma ambazo alisema zilitengenezwa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.