Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yarusha kombora lake Pwani ya Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora lake la masafa ya kati kuelekea Pwani ya nchi ya Japan na kuzua hali ya waziwasi.

Jaribio la kombora nchini Korea Kaskazini
Jaribio la kombora nchini Korea Kaskazini KNS / KCNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hili limetokea wakati Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe akiwa ziarani nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani hatua hii ya Korea Kaskazini, na kumhakikishia Waziri Mkuu  Abe kuwa, Marekani itasimama na nchi yake kwa asilimia 100.

"Nataka mfahamu na kujua kuwa Marekani ipo nyuma ya Japan kwa asilimia 100," alisema Trump.

Serikali ya Korea Kusini nayo imekasirishwa na hatua ya Pyongyang na kuitisha mkutano wa baraza la  usalama jijini Seoul.

Korea Kaskazini imekuwa ikituma majaribio kama haya ya makombora lakini pia silaha zake za Nyuklia, kuonesha uwezo wake wa kijeshi na kutisha nchi jirani zinazoungwa mkono na Marekani.

Nchi hiyo imekuwa pia ikisema ina uwezo wa kurusha kombora la mbali na kuishambulia Marekani ikiwa itachokozwa.

Hata hivyo, watalaam wa Marekani wamekuwa wakisema kuwa Korea Kaskazini bado haina teknolojia ya kurusha kombora hadi katika ardhi yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.