Pata taarifa kuu
UTURUKI-URUSI-USALAMA

Erdogan amtuhumu Gulen kwa mauaji ya balozi wa Urusi

Siku mbili baada ya kuuawa kwa balozi wa Urusi katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema siku ya Jumatano jioni kwamba kijana aliyehusika na kitendo hicho, ambaye ni polisi mwenye umri wa miaka 22, alikuwa mtu wa karibu na imam Fethullah Gulen.

Imamu Fethullah Gulen akiwa ukimbizini nchini Marekani anatuhumiwa na serikali ya Ankara kuhusika katika jaribio la  mapinduzi lililooshindwa mwezi Julai 2016.
Imamu Fethullah Gulen akiwa ukimbizini nchini Marekani anatuhumiwa na serikali ya Ankara kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililooshindwa mwezi Julai 2016. REUTERS/Charles Mostoller
Matangazo ya kibiashara

Nchini Uturuki, uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira ya mauaji ya balozi wa Urusi mjini Ankara Jumatatu Desemba 19 usiku katika nyumba ya sanaa katika mji mkuu wa Uturuki. Serikali ya Uturuki imetangaza siku ya Jumatatu kuundwa kwa tume ya pamoja na Urusi ikiwemo, lakini viongozi walibaini haraka kwamba kulikua na mkono wa imam Fethullah Gulen, adui namba moja wa serikali ya Uturuki, muhusika mkuu katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa la mwezi Julai.

Jumatatu jioni baada ya mauaji ya balozi wa Urusi, wanasiasa walizungumzia kuhusika kwa Fethullah Gulen, mwandishi wa RFI katika mji wa Istanbul, Alexander Billet amearifu. Wasifu wa polisi huyo kijana uliochapishwa katika vyombo vya habari inaonekana kweli kama ni mambo yaliyopangwa. Hata hivyo kuharakia kwa serikali kutangaza chanzo cha mauaji hayo kumezua maswali mengi . Vipi mtu aliye karibu na imam Gullen atakua katika vyomvo vya usalama baada ya jaribio la mapinduzi yaliyohusishwa kiongozi huyo wa kidini

Wachunguzi wa Urusi waliwasili mjini Ankara Jumanne Desemba 20 na hawana imani na hoja ya serikali ya Uturuki. Si lazima kutoa matokeo kabla ya uchunguzi, Ikulu ya Kremlin imesema. Kwa uhusiano wowote ule wa muuaji, awe kutoka kambi ya imam Gullen, Mwislamu mwenye itikadi kali za kidiniau mwendawazimu, shambulio dhidi ya balozi linaonyesha labda jinsi gani vyombo vya usalama vya Uturuki vimesambaratika baada ya miaka mitatu ya kukandamizwa.

Mazishi ya balozi wa Urusi kufanyika mjini Moscow

Mwili wa Andrei Karlov ulirejeshwa nchini Uturuki Jumanne usiku, amearifu mwandishi wa RFI mjini Moscow, Muriel Pomponio. Jeneza la balozi wa Urusi nchini Uturuki lilipokelewa katika uwanja wa ndege na Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, akiambatana na mwenzake wa Uturuki. Sherehe hizo zilirushwa moja kwa moja kwenye runinga ya serikali.

Siku ya Alhamisi, zitatolewa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, mbele ya Vladimir Putin. Kisha sherehe ya kidini itafanyika katika Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin, mauaji hayai pia yanalenga Uturuki, wakati ambapo ilifufua uhusiano wake na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.