Pata taarifa kuu
URUSI-UTURUKI

Wachunguzi wa Urusi waenda Uturuki kubaini kuuawa kwa Balozi wake

Urusi imetuma wachunguzi wake nchini Uturuki kwenda kuchunguza kiini cha afisaa wa Polisi kumpiga risasi na kumuua Balozi wake nchini humo Andrei Karlov.

Andreï Karlov aliyekuwa Balozi wa Urusi nchini Uturuki
Andreï Karlov aliyekuwa Balozi wa Urusi nchini Uturuki Crédits photo : Burhan Ozbilici/AP
Matangazo ya kibiashara

Balozi Karlov, alipigwa risasi na afisa huyo wa polisi aliyetambuliwa kwa jina la Mevlut Mert Altintas mwenye umri wa miaka 22.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema shambulizi hili lililenga kuharibu uhusiano kati ya nchi yake na Urusi.

Karlov mwenye umri wa miaka 62, alishambuliwa na kuuawa wakati alipokuwa anahudhuria maadhimisho ya picha jijini Ankara Jumatatu jioni.

Walioshuhudia wanasema alipigwa risasi wakati akisoma hotuba yake na baada ya tukio hilo, alianguka chini na juhudi za kumwokoa hazikufua dafu.

Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amevalia nadhifu na wakati wa tukio hilo alisikika akizungumza kiarabu na Kituruki akisema Allahu Akbar" (Mungu ni Mkuu).

Hata hivyo, shambulizi hili halitarajiwi kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.