Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAUAJI

Polisi watatu wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga

Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Islamic State wamejilipua Jumapili hii katika mji wa Gaziantep (kusini mashariki mwa Uturuki) wakati wa operesheni dhidi ya ugaidi, shambulio ambalo limesababisha vifo vya polisi watatu na kuwajeruhi wengine kadhaa, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.

Polisi ya Uturuki katika eneo la awali la shambulio la kujitoa mhanga katika mji wa Gaziantep, Agosti 21, 2016.
Polisi ya Uturuki katika eneo la awali la shambulio la kujitoa mhanga katika mji wa Gaziantep, Agosti 21, 2016. AFP/AHMED DEEB
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Gaziantep, mji ulio karibu na Syria, mshambuliaji wa kwanza alilipua mabomu yake wakati ambapo alikua akikaribia kukamatwa wakati wa operesheni iliyoendeshwa na vikosi vya usalamavya Uturukia, amesema Mkuu wa mkoa huo, Ali Yerlikaya, katika taarifa yake kwenye televisheni.

Kwa uchache watu tisa, polisi watano na raia mmoja kutoak Syria, wamejeruhiwa, Mkuu wa mkoa ameongeza.

Mapema Jumapili, vyombo vya habari vya uturuki viliripoti vifo vya washambuliaji wengi wakati wa tukio hili la kwanza, lakini Mkuu wa mkoa na ofisi ya mwendesha mashitaka katika mkoa huo wamesema kuwa mwili wa mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga umepatikana katika eneo la tukio.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, vyombo vya usalama vimeendesha operesheni hii baada ya kupata taarifa kwamba "shambulio la kujitoa mhanga" limekua likiandaliwa katika mji wa Gaziantep dhidi asasi ya utamaduni ya watu jamii ya watu wachache ya Alevi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.