Pata taarifa kuu

Uturuki yataka kudhibiti vilivyo mpaka wake na Syria

Siku mbili baada ya shambulizi lililosababisha fivo vya watu zaidi ya 50 kusini mwa Uturuki, serikali inasema inataka kuonyesha nguvu zake katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic State.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mehmet Cavusoglu, Julai 27, 2015.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mehmet Cavusoglu, Julai 27, 2015. AFP PHOTO / PATRICIA DE MELO MOREIRA
Matangazo ya kibiashara

Katika hali ya kusaidia waasi, Serikali ya Uturuki pia inataka kutoendelea kuzuia waasi wa Kikurdi wa Syria kusonga mbele katika mapambano yake dhidi ya kundi la kigaidi.

"Mpaka wetu unapaswa kusafishwa kikamilifu dhidi ya kundi la IS," alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mehmet Cavusoglu, Jumatatu hii Agosti 22. Kw upande wa mpaka wa Uturuki, mamia ya waasi wa Syria wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki wamekusanywa kwa ajili ya kuuteka mji wa Syria wa Jarablus, unaoshikiliwa na kundi la Islamic State tangu mwaka 2013.

Kauli ya Mehmet Cavusoglu inaja siku mbili baada ya shambulizi lililosababisha vifo vya watu zaidi ya hamsini kusini mwa Uturuki, shambulizi ambalo lilihusishwa kundi la Islamic State. Jumamosi Agosti 20, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika sherehe ya harusi katika mji wa Gaziantep kusini mwa Uturuki, karibu na mpaka wa Syria, na kusababisha vifo vya watu 54.

Shambulizi lilizua hali ya sintofahamu nchini Uturuki, ambayo inakabiliwa na mashambulizi kadhaa yanayohusishwa na kundi la Islamic State tangu mwaka 2015. Vikosi vya Uturuki vinaamini kwamba shambulizi hilo lilitekelezwa na wapiganaji wa kijihadi katika kulipiza kisasi mashambulizi yanayoendeshwa nchini Syria na waasi wa Syria wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.