Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Ankara yaanzisha uchunguzi wa shambulizi la Gaziantep

Serikali ya Uturuki imekua ikijaribu Jumatatu hii kumtambua kijana mdogo aliyehilikisha watu zaidi ya hamsini nchini Uturuki, kwa niabaya kundi la Islamic State.

Magari ya Wagonjwa katika eneo la shambulizi wakati wa harusi katika mji wa Gaziantep,Agost 20, 2016.
Magari ya Wagonjwa katika eneo la shambulizi wakati wa harusi katika mji wa Gaziantep,Agost 20, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema Jumapili kuwa shambulizi l hilo lilitekelezwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekuwa na umri wa miaka ilio kati ya 12 na 14 .

Alisema mwa nyingine tena kuwa taarufa za kwanza zilionyesha kuwa kundi la Islamic State lilihusikia na shambulio hili, ambalo ni baya kabisa mwaka huu.

Wengi wa waliokufa ni watoto au vijana, vyombo vya habari vimearifu na kubaini kwamba watu 29 miongoni mwa watu 44 waliouawa waliotambuliwa mpaka sasa walikuwa chini ya umri wa miaka 18. Afisa mmoja wa serikali ya Uturuki amesema kuwa angalau watu 22 waliouawa walikua watoto walio na umri wa uliyo chini ya miaka miaka 14.

Watu zaidi ya 50 waliuawa na wengine kujeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa bomu wakiwa katika sherehe za harusi Kusini Mashariki mwa Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.