Pata taarifa kuu
UTURUKI-ERDOGAN

Uturuki: maandamano makubwa Istanbul dhidi mapinduzi yaliyotibuliwa

Maandamano makubwa ya kumuunga mkono rais wa Ututuruki Recep Tayyip Erdogan na kulaani mapinduzi yaliyotibuliwa Julai 15 nchini humo yalifanyika Jumapili jioni Agosti 7 katika mji mkuu wa nchi hiyo.

"Mkutano wa demokrasia na mashahidi" uliandaliwa katika eneo la Yenikapi, pembezoni mwa Bahari ya Marmara mjini Istanbul.
"Mkutano wa demokrasia na mashahidi" uliandaliwa katika eneo la Yenikapi, pembezoni mwa Bahari ya Marmara mjini Istanbul. Yasin Bulbul/Presidential Palace
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ambayo walishiriki viongozi wawili wakuu wa upinzani. Rais wa Uturuki alielezea nia yake ya kurejesha adhabu ya kifo, jambo ambalo huenda likasababisha uhusiano mbaya na Ulaya.

Watu milioni tatu hadi milioni nne walivumilia masaa kadhaa katika joto kali wakisubiri hotuba yaRecep Tayyip Erdogan. Hotuba ambayo Rais wa Uturuki mara nyingine tena alitetea nia yake ya kurejesha adhabu ya kifo. Ombi lilikua likitolewa na waandamanaji Jumapili jioni.

"Viongozi wa vyama vyetu vya kisiasa wakohapa na wanajua madai yenu, alisema Rais wa Uturuki. Uhuru wa taifa ni unapewa kipaumbele, kama mnaomba adhabu ya kifo, itapitishwa rasmi na Bunge ! Na kisha nasema mapema mbele yenu, nami nitasahihisha uamuzi huo! "

Mkutano wa Jumapili hii, Agosti 7ulikua kuonyesha jinsi gani raia wanamuunga mkono Rais Recep Tayyip Erdogan. Rais wa Uturuki alitangaza kuwa maandamano ya kila siku katika miji ya Uturuki, ambayo yangelimalizika kwa mkutano huo mkuu, yataendelea hadi Jumatano Agosti 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.