Pata taarifa kuu
UTURUKI-ERODGAN

Erdogan azituhumu nchi za magharibi kusaidia "ugaidi

Rais Erdogan amezituhumu vikali nchi za magharibi tangu jaribio la mapinduzi kushindwa nchini Uturuki, akizitumu nchi hizo kusaidia "ugaidi" na waliotaka kumpindua mamlakani.

Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki.
Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki. Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Kwa bahati mbaya, nchi za magharibi zinasaidia ugaidi na wanaunga mkono walitaka kunipundua," amesema Rais Erdogan katika hotuba yake mjini Ankara, akijibu Marekani na Ulaya amao walimkosoa hivi karibuni kuhusu visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi Julai 15.

"Wale ambao tunafikiria kuwa ni marafiki zetu wanachukua msimamo wa kuunga mkono magaidi," ameongeza Erdogan.

Amesema kuwa mchezo huo wa mapinduzi "uliandaliwa kutoka nje ya nchi." Ankara inamtuhumu mhubiri Fethullah Gulen, anayeishi uhamishoni nchini Marekani kuwa muhusika mkuu wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi,tuhuma ambazo Bw Gulen anakanusha.

Rais Erdogan pia amepinga uamuzi wa Ujerumani ambayo ilimkataza kuwahutubia kwa njia ya video wafuasi wake waliokua walikusanyika Jumapili iliyopita mjini Cologne (magharibi) ili kuunga mkono demokrasia.

Ameituhumu Ujerumani kwa kuweza kuliruhusu kundi la waasi la Wakurdi la PKK, ambalo linachukuliwa na Uturuki kama kundi la kigaidi, lakini pia Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.