Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MATEKA-IS

Australia yaomboleza vifo vya mateka waliouawa

Raia wa Australia wameamka leo Jumanne Desemba 16 wakiweka shada za maua na mishuma mbele ya mgahawa wa Lindt Chocolat katika mji mkuu wa Australia, Sydney, ambapo raia kadhaa walikua walitekwa nyara Jumatatu Desemba 15.

Raia wa Australia wakiweka shada za maua mbele ya mgahawa wa Lindt ambpo waliuawa mateka wawili, katika mji wa Sydney.
Raia wa Australia wakiweka shada za maua mbele ya mgahawa wa Lindt ambpo waliuawa mateka wawili, katika mji wa Sydney. REUTERS/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Polisi ilifaulu kuwaondoa mateka ndani ya mgahawa huo, lakini mateka wawili na mtekaji nyara mmoja waliuawa wakati askari walikua wakirushiana risase na mtekaji nyara huyo.

Wakati huohuo watu wameondolea katika eneo kunakopatikana wizara ya mambo ya nje saa chache ziliyopita kufuatia mfuko moja ambao umeitia mashaka polisi .

Viongozi wa Australia wamegundua baada ya zoezi la kuwaondoa mateka katika mgahawa wa Lindt kuwa utekaji nyara uligharimu maisha ya watu watatu ikiwa ni pamoja na mateka wawili na mtekaji nyara mmoja. Hata hivyo bado wanainchi wana hofu ya kutokea kwa visa vingine kama hivyo.

Raia wa Australia wameghadhibishwa na kisa hicho cha utekaji nyara na huenda hali hiyo ikachochea chuki kati ya jamii mbalimbali nchini humo.

Mtu anaye daiwa kuhusika na kisa hicho cha utekaji nyara ni raia wa Australia mwenye asili ya Iran kutoka jamii ya Waislam, ambaye amekua akinyooshewa kidole kwa kuhusika na vitendo vingi viovu, hususan mauaji ya mkewe na jaribio la ubakaji. Man Haron Monis, alikimbilia Australia mwaka 1996 na kupewa uraia wa nchi hiyo.

Mapema Jumatatu Desemba 15 Asubuhi mateka watano ikiwa ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili walifaulu kuondoka ndani ya mgahawa wa Lindt. Serikali ya Australia imesema mateka waliouawa katika mgahawa huo ni mashujaa.

Mateka hao waliouawa ni Katrina Dawson, mwanasheria, mwenye umri wa miaka 38, mama wa watoto watatu pamoja na Tori Johnson, mwenye umri wa miaka 34, mfanyakazi kwenye mgahawa huo.

Kijana huyo aliuawa wakati aalipokua akjaribu kumpokonya silaha mtekaji nyara. Licha ya kuwa kulikua na majeruhi, mateka 15 waliondoka ndani ya mgahawa wa Lindt bila kuwa na jeraha lolote muilini, baada ya polisi na jeshi kuanzisha operesheni ya kuwaondoa mateka katika mgahawa huo.

Wakati hayo yakiarfiwa, mashrika ya kiislam zaidi ya arobaini yamelani kitendo hicho na kusema kwamba aliyetekeleza kisa hicho hana akili timamu na amekwenda kinyume na misingi ya imani ya Uislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.