Pata taarifa kuu

Mateka wamefaulu kuondoka ndani ya mgahawa wa Lindt Chocolat Australia

Watu watano waliokua wakishikilia mateka na mtu mmoja mwenye silaha katika mgahawa wa lindt Chocolat katika mji mkuu wa Australia, Sydney, wamefaulu kuondoka ndani ya mgahawa huo.

Watu watano waliokua wakishikilia mateka na mtu mmoja mwenye silaha katika mgahawa wa lindt Chocolat katika mji mkuu wa Australia, Sydney, wamefaulu kuondoka ndani ya mgahawa huo
Watu watano waliokua wakishikilia mateka na mtu mmoja mwenye silaha katika mgahawa wa lindt Chocolat katika mji mkuu wa Australia, Sydney, wamefaulu kuondoka ndani ya mgahawa huo REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Bendera nyeusi yenye maandishi ya kiarabu ilitundikwa kwenye moja ya madirisha ya mgahawa huo.

Mtekaji nyara huyo amekua akidai bendera ya kundi la Dola la Kiislam, na amebaini kuwa kuna mabomu manne ambayo alitega katika mji wa Sydney, na hivo kuomba kukutana kwa mazungumzo na Waziri mkuu wa Australia. Hayo yamethibitishwa na mateka ambao wamekua wakishikiliwa na mtekaji nyara huyo kwenye kituo kimoja cha televisheni nchini Australia mara tu baada ya kuachiliwa huru.

Watu hao ambao wamekua wakishikilia mateka ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili. Haijafahamika iwapo ni mateka kweli ambo wameachiliwa huru au ni mbinu walizotumia watekaji nyara hao ili waweze kuondoka ndani ya mgahawa huo, baada ya kuona kuwa wamefikia malengo yao.

Polisi ambayo haina taarifa yoyote kuhusu ni idadi ya watu wa ngapi ambao wanashikiliwa mateka ndani ya mgahawa wa Lindt, wanajaribu kuwahoji watu hao ili kupata taarifa kamili.

“ Mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kuhusu iwapo kuna mtu ambaye ameuawa au kujeruhiwa”, amesema naibu mkuu wa polisi katika jimbo la New South Wales, Catherine Burn.

Burn amebaini kwamba vikosi vya usalama vimekua vikiwasiliana na mtekaji nyara, bila hata hivyo kujua sababu wala kumtambua.

Kwa mujibu wa polisi idadi ya mateka ni chini ya 30. mateka hao wameshikiwa tangu Jumatatu Desemba 15 mapema asubuhi katika mgahawa wa Lindt katikati mwa mji wa Sydney.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.