Pata taarifa kuu
CHINA

Li Keqiang ndiye waziri mkuu mpya wa China

Viongozi nchini China wamemteua Li Keqiang kuwa Waziri Mkuu mpya wa taifa hilo, Li anachukua nafasi ya Waziri Mkuu anayeondoka Wen Jiabao. Li anatarajiwa kuhuduma katika wadhifa huo kwa miaka mitano ijayo lakini huenda muda wake ukaongezwa hadi kufikia miaka kumi.

iphone.malaysiandigest.com
Matangazo ya kibiashara

Li ana umri wa miaka 57 na ana shahada ya uzamivu katika maswala ya uchumi na anatajwa kuwa miongoni mwa watu wa karibu wa Rais anayemaliza muda wake Hu Jintao.

Siku ya Alhamisi wabunge nchini humo walimuidhinisha Xi Jinping mwenye umri wa miaka 59 kuwa Rais wa taifa hilo linalotajwa kama la pili kuwa na uchumi mkubwa duniani.

Uteuzi wa Xi Jinping umekuja miezi minne tangu Xi ateuliwe kuwa Mwenyekiti wa chama tawala cha kikomunisti, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Hu Jintao.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanaona kuwa licha ya China kupata uongozi mpya huenda sera zao za kigeni hazitabadilika kama wengi wanavyotarajia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.