Pata taarifa kuu
INDIA

Waziri mkuu wa India awataka waandamanaji kuwa na subira wakati hatua dhidi ya ubakaji zikichukuliwa

Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh ameendelea kusimama kidete katika kuhakikisha anamaliza maandamano ya kutaka kuchukuliwa hatua kali kwa wabakaji wa mwanafunzi wa udakatari kwa kuwasimamisha kazi maofisa polisi wazembe. 

Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh REUTERS/Andrew Biraj/Files
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu amesema hawatokubali kuendelea kuona hali ya usalama inatetereka kutokana na uzembe wa watu wachache ambao walikuwa na uwezo wa kudhibiti tukio hilo la ubakaji sababu basi hilo lilipita vizuizi kadhaa vya polisi.

Singh amesema waandamanaji wanastahili kuwa watulivu kwa sasa na kuwaachia waendelee kufanya kazi yao ipasavyo katika kuhakikisha wanaimarisha hali ya usalama ya wanawake na watoto wa nchi hiyo.

Jeshi la Polisi nchini India limeendelea kujikuta katika wakati mgumu kukabiliana na maelfu ya waandamanaji ambao wanashinikiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya wabakaji wa binti huyo wa miaka ishirini na tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.