Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Wanajeshi sita wa Uingereza wahofiwa kufa kwenye shambulio la bomu nchini Afghanistan

Wanajeshi sita wa Uingereza wanahofiwa kufa nchini Afghanistan kwenye mji wa Helmand kufuatia gari walilokuwa wakitumia kushambuliwa kwa bomu na watu wasiojulikana. 

Picha ikiwaonesha wanajeshi wa Uingereza walioko kwenye opersheni nchini Afghanistan
Picha ikiwaonesha wanajeshi wa Uingereza walioko kwenye opersheni nchini Afghanistan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imetoa taarifa kuelezea kusikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa miili ya wanajeshi hao bado haijapatikana na kwamba huenda wakawa wameuawa katika shambulio la bomu la kutegwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wanajeshi hao ambao walikuwa wanatumia gari maalumu ambalo linazuia risasi walishambuliwa ghafla wakati wakiwa kwenye doria ya kawaida kwenye mji wa Helmand mji ambao umekuwa ukilengwa na mashambulio ya kujitoa muhanga.

Akizungumza bungeni, waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon ametoa pole kwa familia ambazo zimepoteza ndugu zao kwenye shambulio hilo na kusema kuwa wanajeshi hao wamekufa wakati wakiitumikia nchi yao kishujaa.

Licha ya kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao, waziri mkuu Cameroon ameendelea kusisitiza nchi yake kuendelea kuwaacha wanajeshi wake nchini humo kwa lengo la kutimiza malengo ambayo waliingia nayo awali wakati wakiwasambaratisha wapiganaji wa Taliban.

Kuuawa kwa wanajeshi hao watano wa Uingereza kunafanya idadi ya wanajeshi wa Uingereza waliokufa kwenye vita nchini Afghanistan kufikia mia nne.

Msemaji wa majeshi ya NATO nchini Afghanistan ametoa pole kwa Serikali ya Uingereza na wanajeshi wengine ambao bado wako nchini humo wakishirikiana na majeshi ya NATO kulinda amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.