Pata taarifa kuu
INDIA

Chama tawala nchini India cha Congress chaelekea kupoteza viti vingi kwenye jimbo la Uttar Pradesh

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini India yameanza kutangazwa kwenye majimbo mbalimbali nchini humo huku chama tawala cha Congress kikioneakana kushindwa kwenye jimbo kubwa zaidi la Uttar Pradesh. 

Wasimamizi na wapiga kura nchini India wakati wa upigaji kura kwenye jimbo la Uttar Pradesh
Wasimamizi na wapiga kura nchini India wakati wa upigaji kura kwenye jimbo la Uttar Pradesh Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye matokeo ambayo yameanza kutolewa na tume ya uchaguzi kwenye jimbo hilo yanaonyesha kuwa chama tawala cha Congress kinashika nafasi ya nne huku vyama vingine vya upinzani vikionekana kuibuka kidedea.

Chama cha Bahujan Samaj BSP ambacho kinaongozwa na mwanamama Mayawiti kinaonekana kuongoza kwenye jimbo hilo huku akifuatiwa kwa ukaribu na Mulayam Singh Yadav kiongozi wa chama cha Samajwad.

Rahul Gandhi ambaye aliongoza kampeni za chama tawala kwenye jimbo la Uttar Pradesh amekiri kukubali matokeo ambayo yanatangazwa na tume ya uchagu na kukubali kubebeshwa lawama kutokana na matokeo mabovu.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa huenda matokeo ya mwaka huu yakawa pigo na fundisho kwa chama tawala cha Congress ambacho kimekuwa kikikosolewa kwa sera zake za kujenga uchumi na kukabilina na rushwa.

Gandhi ambaye anatarajiwa kuwa mrithi wa waziri mkuu Manmohan Singh anatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa vyama vilivyoibuka siku za hivi karibuni na kupata umaarufu mkubwa kwa wananchi.

Mpaka sasa matokeo ya awali yanaonyesha kuwa chama cha Congress kimepata viti 27 wakati chama cha The Hindu nationalist Bharatiya Janata kikiongoza kwa viti 44.

Kushindwa kwa chama cha Congress kwenye uchaguzi huo wa majimbo kunaelezwa kumetokana na viongozi wengi akiwemo waziri mkuu wa sasa kukabiliwa na tuhuma za rushwa.

Jimbo la Uttar Pradesh ndilo jimbo ambalo linawapiga kura wengi zaidi ambapo wanakadiriwa kufikia milioni 112.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.