Pata taarifa kuu
India

Wabunge nchini India washindwa kupitisha muswada wa kupambana vita rushwa

Bunge la nchini India limeahirishwa huku wabunge wakishindwa kupigia kura muswada wa sheria ya kupambana na rushwa ambao uliwasilishwa na serikali bungeni kwaajili ya kujadiliwa na baadae kupitishwa na kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani nchini India
Wabunge wa upinzani nchini India RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha jana ambacho kilienda hadi usiku wa manane kilishuhudia hata baadhi ya wabunge wakiuchana muswada ambao umewasilishwa na serikali wakionesha kuchukuziwa na kile walichodai serikali kushindwa kutafisri baadhi ya sheria za rushwa.

Chama cha upinzani nchini India cha Bharatiya Janata BJP kimemtaka waziri mkuu Manmohan Singh kujiuzulu kwa kuwa serikali yake imeshindwa kutekeleza matakwa ya wananchi ya kupambana na rushwa.

Kufuatia hatua hiyo mwanaharrkati Anna Hazare ametangaza kusitisha kwa muda mgomo wake wa kutkula kupinga serikali kushindwa kupitisha sheria hiyo akitishia kurejea tena kwenye mgomo wake siku chache zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.