Pata taarifa kuu
India

Mwanaharakati Anna Hazare na mgomo wa kutokula nchini India

Mwanaharakati mkongwe nchini India Anna Hazare ameanzisha upya mgomo wa kutokula ikiwa ni harakati za kupinga kukithiri kwa rushwa na kuandamana katika mitaa ya Mumbai na kusababisha msongamano wa magari katika barabara lengo kuu likiwa kuhamasisha sheria madhubuti ya kupambana na rushwa nchini humo.

Mwanaharakati wa India Anna Hazare
Mwanaharakati wa India Anna Hazare
Matangazo ya kibiashara

Harakati za mkongwe huyo anayeziendesha kwa mgomo wa kula na kuandamana zimesababisha bunge nchini humo kuanza mjadala wa siku tatu juu ya sheria mpya ya kupambana na rushwa nchini humo.

Mwanaharakati Anna Hazare amesema kupitia waraka wake kuwa muswada huo ni dhaifu na usio na maana hasa katika kipindi hiki ambacho mlolongo wa kashfa za rushwa zinazidi kuiandama serikali ya india na kuiharibia sifa yake.

Tayari ni siku ya 12 tangu mgomo wa mkongwe huyo aliyelenga kampeni za kitaifa kushinikiza serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi ya suala la rushwa.

Tayari kamati yenye watu 9 itaundwa na wawakilishi watakao chunguza na kushughulikia madai ya umma jambo ambalo ni hitaji kubwa la wanaharakati wa kupambana na rushwa kama Hazare na vyama vya upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.