Pata taarifa kuu
INDIA

Moto waua watu zaidi ya 70 hospitalini nchini India

Takribani watu 73 wameungua hadi kufa kufuatia kuzuka na kuenea kwa moto katika hospitali ya AMRI mjini Kalkata mashariki mwa India. 

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa hospitali hiyo umethibitisha kutokea kwa moto huo uliosababisha vifo vya watu 73 wakiwemo wafanyakazi 3 wa hospitali hiyo baada ya kunaswa katika moto na moshi mkali.

Waziri mkuu wa jimbo la Bengal Magharibi Mamata Banerjee amesema tukio hilo ni kosa la jinai na kuahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya hospitali hiyo kwa kutojali taratibu za kiusalama ambapo tayari kesi dhidi ya hospitali hiyo imefunguliwa katika kituo cha polisi.

Mapema mnamo majira ya asubuhi moto huo ulizuka kutokea ghorofa ya saba ya hospitali ya AMRI ambapo vifaa kama mitungi ya kuhifadhia gesi ya oksijeni inatajwa kuwa chanzo cha moto huo.

Vikosi vya uokoaji vinafanya jitihada kuhakikisha vinapambana kuokoa manusura na kutafuta mabaki ya miili ya watu waliopoteza maisha katika hospitali hiyo.

Mashuhuda na manusura wa moto huo wameeleza kuwa vifaa vya tahadhari kama kengele ya hatari na mitungi ya gesi ya kupambana na moto havikuwa na uwezo wa kufanya kazi jambo lililosababisha watu wengi kupoteza maisha baada ya kukata taamaa kwa kushindwa kujiokoa na kuomba msaada.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.