India-Zilzala
Tetemeko la ardhi lauwa watu 36 nchini India
Watu 36 wamefariki dunia Kaskazini Mashariki mwa India katika majimbo ya Himalayan mji wa Nepal, baada ya tetemeko la ardhi lenye richa ya 6 nukta 9 kutokea na kuharibu pia jengo la ubalozi wa Uingereza nchini humo.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Zaidi ya watu sitini walijeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi, ambalo pia limesabisha kubomoka kwa majengo kadhaa nchini katika mji huo wa Nepal na pia kusababisha kukatika kwa umeme na maji katika mji huo.
Serikali inasema inaendelea na shughuli za kuwasaidia wale wote waliothiriwa na tetemeko hilo la ardhi.