Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Colombia: Wapiganaji tisa wa kundi la zamani la FARC wauawa Nariño

Kulingana na jeshi, waasi hao walikuwa wa kundi la Segunda Marquetalia-Alfonso Cano, lililoundwa mnamo mwaka 2019 na Ivan Marquez baada ya kukataa kwa wapiganaji wengine wa FARC kupokonywa silaha. 

Colombia imeendelea kumbwa na machafuko yanayosababishwa na makundi yenye silaha, mengi yakijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na binadamu.
Colombia imeendelea kumbwa na machafuko yanayosababishwa na makundi yenye silaha, mengi yakijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na binadamu. AFP - JOAQUIN SARMIENTO
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yanakuja miezi miwili baada ya kundi hilo - ambalo linaripotiwa kuwa na wapiganaji 1,600 - kutangaza kwamba linataka kuanza mazungumzo ya amani na serikali.

Colombia imeendelea kumbwa na machafuko yanayosababishwa na makundi yenye silaha, mengi yakijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na binadamu.

Hivi karibuni Wizara ya Ulinzi ya Colombia ilitangaza "kuanzisha mashambulizi makubwa" dhidi ya kundi kuu alililojijitenga na kundi la zamani la waasi la FARC katika maeneo matatu (Nariño, Cauca na Valle del Cauca). Bogota inashutumu makao makuu ya jeshi la FARCl (EMC) kwa kukiuka usitishaji mapigano na kuamuru kuanza tena kwa hatua za mashambulizi dhidi yake.

Chini ya mwezi mmoja baada ya kusitishwa kwa mazungumzo ya amani na wapiganaji wa ELN, ni zamu ya maendeleo kwa makundi yaliyojitenga na FARC (Majeshi ya Wanamapinduzi ya Colombia) kutiliwa shaka. Serikali ya Colombia ilitangaza Machi 17 kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano katika maeeo matatu ya nchi yaliyofikiwa na kundi kuu la wapinzani la FARC, baada ya shambulio baya lililotekelezwa na waasi dhidi ya kundi la watu wa asili.

Hapo awali, Rais Gustavo Petro aliripoti shambulio siku moja kabla katika eneo la Toribio, katika eneo la Cauca (kusini-magharibi), akishutumu EMC kwa kuwa katika mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.