Pata taarifa kuu

Haiti: Watu 243 wahamishwa hadi Martinique, wengi wao wakiwa Wafaransa

Zoezi la kuwahamisha raia engine wa kigeni umefanyika katika kisiwa cha Caribbean (Haiti) kilichokumbwa na machafuko na ghasia. Serikali ya Ufaransa imeanzisha safari maalum za ndege kuwezesha raia wa Ufaransa kuondoka Haiti, baada ya kusitishwa kwa safari za anga kwa ndege za kibiashara na nchi hiyo.

Makao makuu ya Bunge huko Port-au-Prince, Jumatatu Machi 25, 2024.
Makao makuu ya Bunge huko Port-au-Prince, Jumatatu Machi 25, 2024. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Kundi la watu 243, wakiwemo raia 163 wa Ufaransa, waliweza kuondoka Haiti, ambako walizuiliwa na maandamano ya kupinga serikali, na lilikuwa likitarajiwa siku ya Ijumaa huko Martinique, alisema gavana wa mkoa huu wa Ufaransa katika Caribbean. Meli tatu kutoka Jeshi la Wanamaji la taifa zinatarajiwa katika Fort-de-France, gavana wa Martinique na kamanda mkuu wa Kikosi cha wanajeshi huko Antilles alisema siku ya Alhamisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Ndani ya ndege kuna watu 243, wakiwemo Wafaransa 163 na wageni 80, nusu yao ni raia wa nchi za Umoja wa Ulaya, kulingana na gavana wa Martinique Jean-Christophe Bouvier. "Raia wa Ufaransa watapewa nafasi ya kurejea Ufaransa mara moja," gavana huyo alibainisha, akiongeza kwamba "wataweza kunufaika na safari ya ndege itakayokodishwa na Wizara ya Mambo ya Ulaya na Mambo ya Nje siku hiyo," alisema Jean-Christophe Bouvier.

Wilaya hiyo pia imebainisha kuwa raia wa kigeni wanaohitaji kuhalalisha visa vyao watakaa kwa usiku mmoja huko Martinique kabla ya uwezekano wa kuondoka katika eneo hilo. Makundi kadhaa ya raia wa Ufaransa yalihamishwa katika siku za hivi karibuni.

Magenge

Haiti, ambayo tayari ni mwaathirika wa mzozo mkubwa wa kisiasa na kiusalama, imekumbwa na ghasia mpya tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, na magenge kadhaa yameungana kushambulia maeneo ya kimkakati huko Port-au-Prince.

Siku ya Jumapili jioni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilitangaza kuanzishwa kwa "safari maalum" za ndege. “Raia wa Ufaransa waliotaka kunufaika na safari maalum za ndege zilizoanzishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Majeshi waliweza kupanda helikopta za Ufaransa ili kujiunga na meli ya kitaifa ya wanamaji ambayo itawasafirisha hadi Fort-de-France hivi karibuni. ", chanzo cha kidiplomasia kimeliambia shirika la habari la AFP. "Zoezi la kuhamisha watu 206 lilifanyika kutumia helikopta kwenda Tonnerre (helikopta kubwa)[...] kati ya Machi 24 na 26 kutoka [...] Port-au-Prince", alibainisha siku ya Alhamisi Nicolas Lambropoulos, kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi huko Antilles.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.