Pata taarifa kuu
KURA YA MAONI

Chile yapinga rasimu ya Katiba mpya

Chile Jumapili ilikataa katiba ya pili iliyopendekezwa ambayo ilikuwa chini ya kura ya maoni. Kwa asilimia 55 ya kura, wananchi wa Chile walisema hapana kwa rasimu ya katibu mpya ambayo imetengenezwa na mrengo wa kulia na mrengo na washirika wao, hivyo kuhitimisha mijadala ya miaka minne, kura zilizorudiwa na kutokuwa na uhakika.

Wafuasi wa kura ya Hapana wakisherehekea matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya inayopendekezwa ya Chile mjini Santiago mnamo Desemba 17, 2023.
Wafuasi wa kura ya Hapana wakisherehekea matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya inayopendekezwa ya Chile mjini Santiago mnamo Desemba 17, 2023. AFP - JAVIER TORRES
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kushindwa mara mbili, Chile kwa hivyo itahifadhi Katiba inayotumika sasa, ile ya udikteta wa Augusto Pinochet. Hapana ilipigiwa 55.75% ya kura, huku Ndio ikipigiwa 44.25% ya kura, kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyochapishwa na Tume ya Uchaguzi (Servel) baada ya 99% ya kura kuhesabiwa.

“Chini ya mamlaka hii, mchakato wa katiba umefungwa. Kuna dharura nyingine,” rais wa mrengo wa kushoto amesema katika hotuba yake katika ikulu ya La Moneda. "Nchi yetu itaendelea na Katiba ya sasa, kwa sababu baada ya mapendekezo mawili ya kikatiba yaliyowasilishwa kwenye kura ya maoni, hakuna iliyofanikiwa kuwakilisha au kuunganisha Chile katika utofauti wake mzuri," ameongeza rais, ambaye aliunga mkono pendekezo la kwanza lililotolewa na mrengo wa kushoto na kuchagua bila kuegemea kwa pendekezo la pili.

Marekebisho ya Katiba ya enzi ya Pinochet (1973-1990), inayozingatiwa kama breki ya mageuzi yoyote ya kimsingi ya kijamii, yalipitishwa ili kukidhi harakati za kijamii za mwaka 2019 dhidi ya ukosefu wa usawa ambao ulisababisha vifo vya watu zaidi yathelathini.

Katika makao makuu ya wanaharakati wa mrengo wa kushoto waliopinga katiba hii mpya, hapakuwa na mimiminiko mikubwa ya furaha, bali kukumbatiana kwa uchache na zaidi ya yote sura ya afueni kwenye nyuso zao, anaripoti mwanahabari wetu Naila Derroisne.

“Wananchi wa Chile walipiga kura kwa wingi dhidi ya rasimu ya katiba ya mrengo mkali wa kulia,” alitangaza waziri wa zamani wa kikomunisti, “rasimu hii ilikuwa hatari kuhusiana na haki zetu ambazo tayari tumeshapata na yenye kupotosha kuhusiana na ile ambayo walipendekeza.”

Njia ya kuchukua

Nchi bado itabaki na Katiba ya sasa ambayo inatoka kwa udikteta na ambayo mrengo wa kushoto unaikosoa vikali. Maria Pardo, alikuwa mjumbe wa baraza la pili la katiba: "Mchakato huu wote umetuonyesha mapungufu na ukimya uliopo katika nakala hii ya 1980 na ni njia gani ya kuchukua sasa".

Rais Gabriel Boric amedokeza kuwa hakutakuwa na jaribio la tatu la kuandika upya Katiba lakini pia ametangaza kwamba ataendeleza ajenda yake muhimu ya mageuzi ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.