Pata taarifa kuu
CHILE-SIASA

Chile yagawanyika baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais

Nchini Chile, wapiga kura walipiga kura kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais jana, Jumapili, Novemba 21, kumchagua mrithi wa mhafidhina Sebastian Piñera. Matokeo yanaonyesha nchi hiyo kuwa imegawanyika.

Nchini Chile, miungano miwili ambayo imegawana madaraka tangu kumalizika kwa udikteta umevunjika na wafuasi  wametawanyika kwa wagombea wawili wenye itikadi kali. Lakini nchi bado imegawanyika.
Nchini Chile, miungano miwili ambayo imegawana madaraka tangu kumalizika kwa udikteta umevunjika na wafuasi wametawanyika kwa wagombea wawili wenye itikadi kali. Lakini nchi bado imegawanyika. ERNESTO BENAVIDES AFP
Matangazo ya kibiashara

Wachile wakiongozwa na mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia José Antonio Kast, wakili mwenye umri wa miaka 55 ambaye ni mshirika wa Pinochet. Mgombea mwengine ni Gabriel Boric, ambaye anatimiza umri wa miaka 35, kutoka cjama cha mrengo wa kushoto.

Tunaweza kusema kuwa Chile ilifungua ukurasa katika historia yake ya kisiasa jana, ameandika mwandishi wetu maalum nchini Chile, Raphaël Moran. Miungano miwili ambayo iligawana madaraka tangu kumalizika kwa utawala wa udikteta imevunjika na wafuasi wamegawanyika kwa wagombea wawili wenye itikadi kali. Mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia José Antonio Kast, kwanza, anadai kuwa ni mrithi wa Pinochet, na ambaye ameweza kurudisha kura za za mrengo wa kulia wa serikali, iliyodhoofishwa sana baada ya rais Piñera kupoteza imani kwa raia.

Kast anaingia katika duru ya pili ya uchaguzi kwa karibu 28% ya kura: alifanya kampeni ya kurejea kwa utulivu mitaani, dhidi ya haki ya kutoa mimba na anajitokeza kama mgombea wa uhuru dhidi ya ukomunisti. Mbele ya wafuasi wake, waliokusanyika katika vitongoji vya Santiago, mgombea huyo wa siasa kali za mrengo wa kulia alisisitiza usalama kwa mara nyingine na kumshambulia mshindani wake Gabriel Boric, "mgombea pekee wa urais ambaye anatetea njia mbadala ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya na wahalifu," chaguo pekee ambalo litakomesha ugaidi. Gabriel Boric na Chama cha Kikomunisti wamesema wenyewe kwamba wanataka kukosekana kwa utulivu katika nchi yetu, na kwamba wanataka kuendelea kwenye njia ya chuki, kutovumiliana na uharibifu. Hii lazima iishe, "amesema Justine Fontaine akihojiwa na mwandishi wetu huko Santiago.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.