Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Mlipuko wa gari kwenye daraja linalounganisha Marekani na Canada waua watu wawili

Watu wawili wamefariki Jumatano kufuatia mlipuko wa gari kwenye daraja la mpaka kati ya Canada na Marekani, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amezungumza juu ya "hali mbaya" katika Bunge. “Hali kwa kweli ni mbaya . Gari limelipuka kwenye daraja la Rainbow,” amesema.

Vikosi vya usalama vyazuia ufikiaji kwenye Daraja la Rainbow kwenye mpaka wa Marekani mnamo Novemba 22, 2023.
Vikosi vya usalama vyazuia ufikiaji kwenye Daraja la Rainbow kwenye mpaka wa Marekani mnamo Novemba 22, 2023. AP - Carolyn Thompson
Matangazo ya kibiashara

Daraja la mpaka kati ya Marekani na Canada limefungwa Jumatano kufuatia mlipuko wa gari kwenye mpaka wa Marekani karibu na Maporomoko ya Niagara, mamlaka imesema. Watu wawili walikufa katika mlipuko huo, kulingana na vyombo vya habari vya Amerika. Fox News inaripoti shambulio la kigaidi lililoshindwa.

"Hali ni mbaya katika Maporomoko ya Niagara. Gari limelipuka kwenye Daraja la Rainbow,” mkuu wa serikali ya Canada ameeleza Bunge. "Bado kuna maswali mengi na tunajaribu kupata majibu haraka iwezekanavyo," ameongeza.

Polisi wa Shirikisho (FBI) "wanachunguza mlipuko huo wa gari kwenye Daraja la Rainbow, kivuko cha mpaka kati ya Marekani na Canada katika Maporomoko ya Niagara," ofisi ya FBI imeandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). Taarifa inabainisha kuwa hali ni "mbaya".

Gavana wa Jimbo la New York Kathy Hochul amesema kwenye mtandao wa X kuwa polisi katika jimbo lake inafanya kazi kwa ushirikiano na  kitengo kinacho pambana dhidi ya ugaidi kukaguwa maeneo maeneo yote yanayoingia katika jimbo lake la New York. Ameongeza kuwa atazuru eneo la tukio.

Manisoa ya Jiji la Marekani la Niagara Falls inasema kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba Daraja la Rainbow limefungwa "mpaka." Kwa upande wa Canada, polisi wa eneo hilo imesema ina "kuhusika kidogo" katika kesi hiyo kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.