Pata taarifa kuu

Canada: Vituo vya kulea watoto Alberta vyakumbwa na wimbi la maambukizi ya bakteria ya E.coli

Canada kwa sasa inakabiliwa na mojawapo ya visa vyake vibaya zaidi vya maambukizi ya bakteria ya E.coli. Tangu Septemba 4 huko Calgary, katika jimbo la Alberta, watoto wadogo 339 wameathiriwa. Waziri Mkuu ametangaza tu fidia ya kifedha kwa wazazi, lakini pia anataja mabadiliko yajayo katika sheria.

Wimbi la maambukizi ya bakteria ya E.coli linakumba vituo vya kulelea watoto katika jimbo la Alberta nchini Canada.
Wimbi la maambukizi ya bakteria ya E.coli linakumba vituo vya kulelea watoto katika jimbo la Alberta nchini Canada. AFP - INA FASSBENDER
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Quebec, Pascale Guéricolas

Takriban wiki mbili baada ya visa vya kwanza vya maambukizi, idadi ya vituo vya kulelea watoto walioathiriwa na bakteria ya E.coli inaendelea kuongezeka huko Calgary, katika jimbo la Alberta. Jumamosi Septemba 16, watoto 12  walilazwa hospitalini, kati ya zaidi ya 300 walioathirika.

Wengi wanakabiliwa na matatizo yanayoathiri damu na figo zao. Licha ya utafiti wa kina, chanzo halisi cha mlipuko wa bakteria bado hakijajulikana. Kwa upande mwingine, ripoti za ukaguzi zilionyesha kuwa kuna mashaka kuwa chanzo cha bakteria hiyo kinapatikana katika jiko kuu. Hapa ndipo milo hutayarishwa kwa vitalu na vituo vya shule ya awali. Kuna hata harufu ya maji taka.

Akihusishwa na wazazi kadhaa ambao walizindua hatua za pamoja za kisheria, Waziri Mkuu wa Alberta ameahidi hatua. Pia ametoa euro 1,300 kama fidia kwa familia ambazo zinapaswa kuchukua likizo ya kazi ili kutunza watoto wao. Hadi sasa, hakuna kanuni sahihi kuhusu utunzaji wa chakula katika vituo vya kulelea watoto katika jimbo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.