Pata taarifa kuu

Canada: Zaidi ya heka milioni 10 zateketea kwa moto, sawa na ukubwa wa Ureno

Canada ilivuka Jumamosi Julai 15 kiwango cha heka milioni 10 zilizoteketea kwa moto tangu mwanzoni mwa mwaka. Kutokana na ukubwa wa moto wa misitu, mamlaka inaonekana kuzidiwa nguvu.

Moshi mwingi msituni na maeneo yaliyoteketea kwa moto karibu na Lebel-sur-Quevillon, Quebec, Jumatano, Julai 5, 2023.
Moshi mwingi msituni na maeneo yaliyoteketea kwa moto karibu na Lebel-sur-Quevillon, Quebec, Jumatano, Julai 5, 2023. AP - Adrian Wyld
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Montreal, Justine Cohendet

Ili kutoa wazo la ukubwa wa hali hiyo, kwa sasa kuna visa 570 vya moto wa nyika ambao haudhibitiwi nchini Canada. Zaidi ya matukio 900 ya moto unawaka kwa jumla.

Maafisa wa kikosi cha Zima moto wanajaribu kudhibiti moto huu, lakini ni vigumu, hasa kwa sababu kuna moto mwingi unaowaka kwa wakati mmoja. Heka milioni kumi za misitu zimeteketea kwa moto huu tangu mwanzoni mwa mwaka, sawa na ukubwa wa Ureno, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini humo.

Quebec ndio mkoa ulioathiriwa zaidi, na zaidi ya heka milioni 4 zimeteketea kwa moto. Eneo la Kaskazini mwa jimbo hilo linakabiliwa na ukame mkubwa. Mashariki mwa James Bay, msitu wa boreal umeharibiwa na moto wa nyika mkubwa zaidi katika historia ya Quebec, moto ambao unachukua zaidi ya heka milioni moja ambao ulilazimisha wakaazi wa jiji la Radison kuhamishwa.

Katika picha hii ya tarehe 18 Juni 2023 iliyotolewa na Usalama wa Umma Canada, wazima moto wa Ufaransa wanajaribu kudhibiti moto wa msitu karibu na Chibougamau, Quebec (Canada).
Katika picha hii ya tarehe 18 Juni 2023 iliyotolewa na Usalama wa Umma Canada, wazima moto wa Ufaransa wanajaribu kudhibiti moto wa msitu karibu na Chibougamau, Quebec (Canada). © Public Safety Canada / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.