Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Guatemala: Wasiwasi watanda baada ya kusimamishwa kwa zoezi la kutangaza matokeo ya uchaguzi

Kusitishwa kwa zoezi la kutangaza matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Guatemala kulizua shaka juu ya kura hiyo na Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya mataifa ya Amerika wameelezea wasiwasi wao siku ya Jumapili Julai 2.

Mbunge Bernardo Arevalo, hapa siku moja baada ya duru ya kwanza katika Jiji la Guatemala, aliwashangaza wengi kwa kupata 11.77% ya kura.
Mbunge Bernardo Arevalo, hapa siku moja baada ya duru ya kwanza katika Jiji la Guatemala, aliwashangaza wengi kwa kupata 11.77% ya kura. REUTERS - JOSUE DECAVELE
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya uchaguzi wa kwanza wa rais yameshangaza wengi nchini Guatemala. Wagombea urais wawili kutoka chama cha Democratic walijikuta wakiongoza kati ya wagombea 22 wa kiti cha urais katika duru ya kwanza, iliyogubikwa na idadi kubwa ya watu waliojizuia kupiga kura na idadi kubwa ya kura batili. Mpasuko unaojiri baada ya mihula mitatu mfululizo ya marais kutoka mrengo wa kulia: Otto Perez (2012-2015), Jimmy Morales (2016-2020 na rais anayemaliza muda wake Alejandro Giammattei.

Duru ya pili imepangwa kufanyika Agosti 20, lakini Mahakama ya Katiba, mahakama ya juu zaidi nchini humo, iliamuru Mahakama ya Juu ya Uchaguzi siku ya Jumamosi Julai 1, kusimamisha kwa muda urasimishaji wa matokeo ya Juni 25. Vyama tisa vya mrengo wa kulia, ikiwa ni pamoja na chama cha rais anayeondoka Alejandro Giammattei, Vamos, viliwasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama hiyo. Vyama hivyo vilitaja "hatari na tishio lililo karibu" la kuona nyadhifa zikitolewa kabla ya madai ya "makosa" ya kura kuwasilishwa kwa tume za uchaguzi, kulingana na Mahakama.

Sandra Torres, mke wa zamani wa rais wa zamani wa mrengo wa kushoto Alvaro Colom (2008-2012) na mgombea ambaye alishindwa mara kadhaa, alipata 15.86% ya kura. Mbunge Bernardo Arevalo, mtoto wa rais wa kwanza wa nchi aliyechaguliwa kidemokrasia, Juan José Arevalo (1945-1951), alishangaza wengi kwa kupata 11.77%. Aliwekwa katika nafasi ya 8ᵉ na 2.9% ya nia ya kupiga kura katika uchunguzi wa hivi punde wa Taasisi ya Prodatos.

Mahakama ya Kikatiba iliomba kuitishwa kwa "kikao cha mapitio ya kura". Mizozo na kukashifu madai ya udanganyifu katika uchaguzi huo vilianza siku moja baada ya duru ya kwanza. "Uchaguzi lazima ufanyike upya", alisema Ijumaa wakili wa chama cha Valor (ujasiri kwa Kifaransa), chama cha Zury Rios, binti wa dikteta wa zamani Efrain Rios Montt (1982-1983) na kushika nafasi ya sita katika duru ya kwanza. Chama hiki kilishutumu "udanganyifu" kwa kudhaniwa kubadilishwa kwa kura elfu moja au 0.82% ya jumla.

Siku ya Jumapili, ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya pamoja na Jumuiya ya mataifa ya Amerika (OAS) ulitoa wito wa kuheshimu matakwa ya wapiga kura.

Katika taarifa, ujumbe wa EU ulitoa wito kwa "taasisi za mahakama na vyama vya kisiasa kuheshimu matakwa ya wazi ya raia yaliyoonyeshwa kwa uhuru katika uchaguzi wa Juni 25". Mnamo Juni 27, siku mbili baada ya kupiga kura, EU ilionya dhidi ya "kuzorota kwa utawala wa sheria na uhukumu wa matukio ya uchaguzi kwa madhumuni ya kisiasa tu", ikisisitiza "kujitolea kwa nguvu kwa raia kwa demokrasia na maadili ya kiraia".

OAS ilitoa wito kwa "mamlaka ya nchi, Bunge, mahakama na serikali, kuheshimu mgawanyo wa mamlaka, uadilifu wa mchakato wa uchaguzi, pamoja na kazi na mahitimisho yaliyofanywa katika mchakato huu". "Heshima ya kujieleza kwa watu kupitia kura ni muhimu ili kudumisha imani kamili ya raia na jumuiya ya kimataifa katika upigaji kura," liliongeza shirika la kikanda katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Guatemala ni mojawapo ya nchi zisizo na usawa katika Amerika ya Kusini, imesema Benki ya Dunia, ikiwa na wakazi milioni 10.3 kati ya milioni 17.6 wanaoishi chini ya mstari wa umaskini na mtoto mmoja kati ya wawili wanaosumbuliwa na utapiamlo wa muda mrefu, kulingana na Umoja wa Mataifa.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.