Pata taarifa kuu

Takriban wahamiaji 1,300 wa Amerika Kusini wakamatwa nchini Mexico

Mexico inakabiliana na wahamiaji wasio na vibali wanaingia katika nchi hiyo ya Amerika Kusini wakijaribu kufika nchini Marekani. Katika kipindi cha saa 24, karibu wahamiaji 1,300 wamekamatwa na polisi, kulingana na mamlaka ya nchi hii.

Askari wa Kikosi cha Kulinda Mpaka wakiwakamata wahamiaji waliokuwa wamewasili Yuma, Arizona mnamo Februari 5, 2022, baada ya kuvuka mpaka wakitokea Mexico.
Askari wa Kikosi cha Kulinda Mpaka wakiwakamata wahamiaji waliokuwa wamewasili Yuma, Arizona mnamo Februari 5, 2022, baada ya kuvuka mpaka wakitokea Mexico. AP - Elliot Spagat
Matangazo ya kibiashara

Polisi iliingilia kati Alhamisi kwenye barabara inayotumiwa na wahamiaji kusini mwa nchi, kwenye mpaka na Guatemala, hadi kskazini kwenye mpaka na Marekani.

Wahamiaji hao waliokamatwa walikuwa wakisafiri wakiwa wamefichwa kwenye malori, pia wakiwa wamefichwa kwenye matangi tupu ya maji yaliyopakiwa kwenyemagari madogo. Wengine walikuwa wamepanda mabasi ya watalii.

Miongoni mwa waliokamatwa ni zaidi ya wanaume 700, wanawake 300 na karibu watoto 200, 165 kati yao hawakuandamana na wazazi wao. Hakuna hata mmoja wa wahamiaji hawa aliye na kibali halali kinachomruhusu kuingia na kutoka Mexico.

Wengi wao wanatoka Amerika ya Kati: Wa Honduras, Guatemala na Salvador wamekuwa wakikimbia ghasia na umaskini kwa miaka kadhaa. Lakini zaidi ya wahamiaji 300 wa Colombia pia ni miongoni mwa waliokamatwa.

Mwaka jana, karibu wahamiaji milioni mbili walikamatwa katika mpaka wa Mexico na Marekani. Mexico tangu wakati huo imeimarisha udhibiti.

Maelfu ya wahamiaji kwa sasa wanashikiliwa huko Tapachula, kusini mwa nchi hiyo. Baadhi wameamua kukaa kimya, wengine wamegoma kula. Wanadai pasi za kibinadamu ili waweze kufika Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.