Joe Biden azungumza na Justin Trudeau na kutoa msaada dhidi ya moto nchini Canada
Rais wa Marekani Joe Biden ametoa msaada wake kwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau wakati wa mazungumzo ya simu kuhusu "moto mbaya na wa kihistoria" unaoikumba Canada, Ikulu ya White House imebaini leo Alhamisi, Juni 8, 2023.
Imechapishwa:
"Rais ameagiza timu yake kupeleka uwezo wote wa shirikisho wa kuzima moto ambao unaweza kusaidia haraka kuzima moto unaoathiri wananchi wa Canada na Marekani," White House imebaini katika taarifa, huku moshi kutoka kwa moto huo ukifunika sehemu kubwa ya kaskazini-mashariki mwa Marekani.
"Mamia ya maafisa wa kikosi cha Zima moto wa Marekani wamewasili hivi punde nchini Canada na wengine zaidi wako njiani," Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alitangaza Jumatano jioni, baada ya kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden.
"Mioto hii hutokea mara kwa mara kwa sababu ya mabadiliko ya Tabia nchi," Justin Trudeau amesema kwenye Twitter.