Pata taarifa kuu
MAREKANI- SIASA

Joe Biden: Ni aibu kubwa wabunge kushindwa kumchagua Spika Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden, amesema ni aibu kwa wabunge mpaka sasa kushindwa kumchagua Spika, baada ya mgombea wa chama cha Republican, Kevin McCarthy, kwa mara ya tano, kushindwa kupata uungwaji mkono wa kura 218 kutoka kwa wabunge wa chama chake ili kuibuka mshindi.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden AP - Achmad Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inadhalilisha sana nchi yetu na ina maanisha kwamba bunge limeshindwa kabisa kufanya kazi yake na hii ni aibu kubwa sisi ni taifa kubwa duniani.” amesea rais Biden.

Wabunge kwa siku ya tatu leo, wanakutana kujaribu tena kumchagua Spika, wakati huu wabunge 20 wenye msimamo mkali, kutoka chama cha Republican wanaomyima ushindi mgombea wao, wakitarajiwa kuendelea na msimamo huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.