Pata taarifa kuu
MAREKANI- SIASA

Vikao wa vya bunge nchini Marekani kuanza leo Jumanne

Kikao cha 118 cha bunge la wawakilishi nchini Marekani, kinafunguliwa hii leo, macho na masikio yakielezwa kwenye zoezi la kumchagua Spika mpya kuona iwapo mbunge wa Republican, Kevin McCarthy kutoka California anaweza kushinda nafasi hiyo. 

Bunge la Congress nchini Marekani
Bunge la Congress nchini Marekani © AP/J. David Ake
Matangazo ya kibiashara

Kushinda nafasi hiyo katika bunge hilo la wawakilishi 435-anapaswa kushinda kwa kura 218. 

Uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita, chama cha Republican ushindi mwembamba katika bunge hilo wa viti 222 dhidi ya 213 kutoka chama cha Democratic. 

Spika anayemaliza muda wake Nancy Pelosi amekuwa kiongozi wa chama cha Democratic katika bunge hilo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.