Pata taarifa kuu

Haiti kupata msaada mpya wa Canada na Vikwazo Dhidi ya Rais wa Zamani Martelly

Canada imetangaza msaada mpya kwa Haiti na vile vile kumwekea vikwazo rais wa zamani wa Haiti Michel Joseph Martelly na Mawaziri Wakuu wawili wa zamani Laurent Lamothe na Jean-Henry Céant, wanaotuhumiwa kunufaika na kazi ya magenge yenye silaha.

Pamoja na mawaziri wawili wa zamani, Rais wa zamani wa Haiti Michel Martelly anatuhumiwa kufadhili magenge yenye silaha.
Pamoja na mawaziri wawili wa zamani, Rais wa zamani wa Haiti Michel Martelly anatuhumiwa kufadhili magenge yenye silaha. Reuters/Swoan Parker
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na utawala wa Canada, watu hawa hutoa msaada wa kifedha kwa magenge yenye silaha ambayo yanawatia hofu raia wa Haiti. Tangazo la vikwazo hivi ni pamoja na vingine vilivyochukuliwa wiki jana dhidi ya mawaziri walio madarakani, Kiongozi wa Bunge la Seneti, wabunge wa zamani na viongozi wa magenge. Nchini Haiti, vikwazo hivi vimekaribishwa na raia kama mwanga wa matumaini.

Kwa upande wake, Me Frantz Mon Fils ameipongeza Canada kwa hatua hizi ambazo zinalenga kusaidia Haiti kujiondoa mikononi mwa wanasiasa wake wafisadi. Mwanaharakati huyo ametangaza maandamano ili kuhimiza vyombo vya sheria nchini Haiti kushughulikia kesi hii.

Canada pia imetangaza vifurushi kadhaa vya misaada kwa Haiti kwa jumla ya dola milioni 16.5 za Canada, hasa kusaidia nchi hiyo kukabiliana na janga la kipindupindu na kupambana dhidi ya ufisadi na kutokujali. Dola milioni nane zitalipwa ili kukidhi mahitaji ya watu walioathiriwa na mzozo wa usalama, afya na chakula.

Msaada huu ni "muhimu kutoa maji, chakula na usaidizi wa kiafya unaohitajika kupambana na kipindupindu", amesema Waziri Mkuu Justin Trudeau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.