Pata taarifa kuu
EL Salvador

Rais wa zamani wa Salvador aagizwa kukamatwa

El Salvador imeagiza kukamatwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Salvador Sanchez Ceren na maafisa tisawa utawala wa zamani katika uchunguzi kuhusu madai ya kujitajirisha kinyume cha sheria na ufisadi, ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa jamhuri imesema.

Rais wa zamani wa El Savador, Salvador Sanchez Ceren.
Rais wa zamani wa El Savador, Salvador Sanchez Ceren. REUTERS/Henry Romero
Matangazo ya kibiashara

Salvador Sanchez Ceren hayupo nchini El Salvador, kulingana na ofisi ya mwendesha mashitaka wa jamhuri, lakini maafisa sita wa utawala wa raisMauricio Funes, madarakani tangu mwaka 2009 hadi 2014, wamekamatwa. Wakati huo, Salvador Sanchez Ceren alikuwa makamo rais.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa jamhuri imetangaza kwamba watu wanaolengwa na uchunguzi wanatafutwa kwa utakatishaji pesa na ufisadi baada ya kupokea fedha kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.