Pata taarifa kuu
MAREKANI-POLAND-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Trump atangaza kuwahamishia Poland askari wa Marekani waliopo Ujerumani

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba askari wa Marekani waliopo nchini Ujerumani atawahamishia nchini Poland.

Rais Donald Trump alimpokea mwenzake wa Poland Andrzej Duda katika Ikulu ya White House. Juni 24, 2020.
Rais Donald Trump alimpokea mwenzake wa Poland Andrzej Duda katika Ikulu ya White House. Juni 24, 2020. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ishara kubwa kwa mwenzake wa Poland siku nne kabla ya uchaguzi hatari ambapo kiongozi huyo atatetea nafasi yake kwa muhula wa pili. Rais wa Poland Andrzej Duda ndiye mgeni wa kwanza wa heshima kupokelewa katika Ikulu ya White tangu kuzuka kwa janga la Corona.

"Rais wa Poland amefanya kazi nzuri na nadhani atafanikiwa sana katika uchaguzi ujao," amesema Donald Trump.

Rais huyo wa Marekani amempongeza mwenzake wa Poland, akisema tofauti na Ujerumani, Poland itaheshimu majukumu yake ya kifedha kwa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO.

"Tutahamisha askari wetu kutoka Ujerumani kwenda Poland. Tutapunguza vikosi vyetu nchini Ujerumani hadi 25,000. Ujerumani inalipa sehemu ndogo ya kile kinachotakiwa kulipwa, huko ni kujipenda, ni hali isiyokubalika. Ninatumia neno hilo, kujipenda. Kwa hivyo tutaondoa wanajeshi wetu nchiniUjerumani. Wengine watarudi nyumbani, wengine watapelekwa mahali pengine huko Ulaya, pamoja na Poland", amebaini rais Trump.

Tangazo ambalo linaonyesha uungwaji mkono wa Donald Trump kwa ais Duda siku nne kabla ya uchaguzi wa urais. Lakini rais wa Marekani amesema hana nia yoyote ya kuingilia uchaguzi huo. "wananchi wa Poland wanajua kizuri alichowafanyia.kwa hiyo haitaji msaada wangu. atashinda uchaguzi, " amesema rais wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.