Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MAREKANI-USALAMA-USHIRIKIANO

Berlin yaona ni muhimu kuepo kwa vikosi vya Marekani nchini Ujerumani

Uwepo wa vikosi vya Marekani nchini Ujerumani ni muhimu kwa usalama wa Marekani na Ulaya, amesema Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas leo Jumanne.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas katika mkutano na waandishi wa habari huko Berlin, Juni 5, 2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas katika mkutano na waandishi wa habari huko Berlin, Juni 5, 2020. Michael Kappeler/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Berlin inakuja siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa anataka kupunguza idadi ya askari wa Marekani wlioko nchini Ujerumani.

"Tunaamini kwamba uwepo wa majeshi ya Marekani nchini Ujerumani ni muhimu kwa usalama sio tu wa Ujerumani lakini pia kwa usalama wa Marekani na hasa kwa usalama wa Ulaya, " Maas amesema wakati wa ziara yake nchini Poland.

Jumatatu wiki hii rais wa Marekani alibaini kwamba uwepo wa askari 52,000 wa Marekani nchini Ujerumani kwa sasa, ni "gharama kubwa kwa Marekani".

Rais Donald Trump ametangaza kwamba atapunguza idadi ya wanajeshi wa nchi yake waliopo Ujerumani hadi kufikia 25,000, akimshutumu mshirika huyo wa karibu wa Marekani kwa kushindwa kukidhi matakwa ya kupandisha bajeti ya ulinzi ya Jumuiya ya NATO, na pia kuitumilia Marekani kwenye mambo ya biashara.

Hata hivyo kuna kati ya wanajeshi 34,000 na 35,000 pekee wa kudumu walioko Ujerumani, kulingana na takwimu rasmi kutoka Pentagon. lakini, idadi hii inaweza kuongezeka hadi 52,000 kutokana na kuwa kuna askari wengi ambao walikuja kufuata mafunzo ya kijeshi nchini humo.

Kupunguzwa kwa wanajeshi 9,500 kunatajwa kuwa hatua kubwa inayodhihirisha mpasuko baina ya washirika hawa wawili wakubwa kibiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.