Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-CHINA-USALAMA-USHIRIKIANO

Marekani yataka China kushirikishwa kwenye mkataba mpya kuhusu silaha

China inapaswa kushirikishwa katika mazungumzo yoyote ya baadaye juu ya udhibiti wa silaha kati ya Marekani na Urusi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov Ijumaa wiki hii.

Mike Pompeo amemwaambia mwenzake wa Urusi Sergueï Lavrov kwamba China inapaswa kushirikishwa katika mazungumzo yoyote ya baadaye juu ya udhibiti wa silaha kati ya Marekani na Urusi
Mike Pompeo amemwaambia mwenzake wa Urusi Sergueï Lavrov kwamba China inapaswa kushirikishwa katika mazungumzo yoyote ya baadaye juu ya udhibiti wa silaha kati ya Marekani na Urusi © Pavel Golovkin/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mazungumzo yao ya simu, Mike Pompeo amemwaambia mwenzake kwamba "mazungumzo yoyote ya baadaye kuhusu udhibiti wa silaha yanapaswa kufanyika kwa maono ya Rais (Donald) Trump kwa makubaliano ya pande tatu kuhusu udhibiti wa silaha ambayo yanajumuisha pia Urusi na China, "Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Morgan Ortagus, amesema katika taarifa.

China, ambayo inakadiriwa kuwa na silaha 300 za nyuklia, kiwango kidogo kuliko Marekani na Urusi, imefutilia mbali mazungumzo hayo.

Mwaka uliyopita Donald Trump alipendekeza kwamba Marekani, Urusi na China zinapaswa kujadili makubaliano yanayo lenga kuchukua nafasi ya mkataba mpya wa START wa mwaka wa 2010 unaoweka kikomo kwene kiwango cha silaha za nyuklia za Marekani na Urusi.

Mkataba huu wa START utamalizika mwezi Februari 2021 isipokuwa ikiwa nchi hizo mbili zitakubali kuongeza muda iwa miaka mitano, jambo ambalo Urusi imependekeza rasmi.

Sergey Lavrov ametoa pendekezo hilo wakati wa mazungumzo ya simu na Mike Pompeo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.