Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Ung'atuzi dhidi ya Donald Trump: Wademocrat waweka kanuni za utaratibu

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha azimio linaloweka sheria za utaratibu wa kumng'atua madarakani Donald Trump. Hatua mpya rasmi katika maagizo yanayoendelea kufanywa dhidi ya rais wa Marekani.

Baraza la Wawakilishi limethibitisha hatua mpya kuelekea mchakato wa kumng'a mamlakani Donald Trump, Alhamisi, Oktoba 31, 2019.
Baraza la Wawakilishi limethibitisha hatua mpya kuelekea mchakato wa kumng'a mamlakani Donald Trump, Alhamisi, Oktoba 31, 2019. REUTERS/Tom Brenner
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Democratic, ambacho kinashikilia viti vingi katika Baraza la Wawakilishi nchini Marekani, hakikupata usumbufu wa kupitisha azimio hilo, na hivyo kufungua hatua mpya katika uchunguzi wa kesi ya mazungumzo ya simu baina ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine.

Mazungumzo hayo ya simu yamewafanya wabunge kutoka chama cha upinzani cha Democrats kuanzisha uchunguzi rasmi wenye lengo la kumng'oa madarakani bw Trump.

Wabunge wa Democrats wanamshutumu Trump kwa kutaka usaidizi kutoka kwa taifa la kigeni ili kumuangamiza hasimu wake wa kisiasa.

Mara tu baada ya kura kupigwa, Donald Trump alionyesha kutoridhika kwake kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa ya White House inathibitisha kuwa, mnamo Julai 25, Trump alimuomba rais Volodymyr Zelenski kumchunguza makamo wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden ambaye anasaka tiketi ya urais kupitia chama cha Democrats, ambaye mtoto wake alikuwa akifanya kazi na shirika la gesi la Ukraine.

Bw Trump anakanusha kuwa alizuia msaada wa kijeshi kwa Ukraine kama njia ya kuishinikiza nchi hiyo kumsaidia kumchafua adui wake wa kisiasa, bw Biden.

Taarifa juu ya mazungumzo hayo ya simu ilitolewa na mtoa taarifa wa siri.

Zaidi ya miaka 20 baada ya kura ya mwisho ambayo ilifungua utaratibu kama huo dhidi ya Bill Clinton, mpango huo ulipitishwa kwa kura 232 dhidi ya kura 196.

Wabunge wa Chama cha Republican wamepinga mpango huo na kuonyesha uungwaji wao mkono kwa Rais Donald Trump.

Hivi karibuni Bwana Trump alikiri kuwa alimzungumzia Joe Biden na Bwana Zelensky lakini akasema alikuwa tu akijaribu kuitaka Ulaya iingilie kati kutoa msaada kwa kuitishia kusitisha msaada wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.