Pata taarifa kuu
VENEZUELA- URUSI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Urusi yashtumu Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela

Urusi ambayo ni mshirika mkuu wa Nicolas Maduro kimataifa imeonekana kwa mara nyingine kumuunga mkono rais huyo. Urusi imeishtumu Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov katika mkutano na waandishi wa habari Moscow Januari 16, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov katika mkutano na waandishi wa habari Moscow Januari 16, 2019. REUTERS/Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Urusi inakuja siku chache baada ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya kampuni moja ya mafuta ya Venezuela.

Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, ameshtumu "mwenendo usiokubalika" wa hatua za Marekani dhidi ya sekta ya mafuta nchini Venezuela.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Nicolas Maduro imeanzisha mbinu mpya ya kukabiliana na kiongozi mkuu wa upinzani, Spika wa bunge la nchi hiyo Juan Guaido, ambaye hivi karibuni amejitangaza kuwa ni rais wa mpito wa Venezuela.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tarek William Saab, mshirika wa karibu wa Nicolas Maduro, ameanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani. Bw Saab ameomba Mahakama Kuu (TSJ), taasisi iliyo mikononi mwa Nicolas Maduro, kupiga marufuku Juan Guaido kuondoka nchini Venezuela na kuzuia akaunti zake za benki.

Hivi karibuni Bw Guaido alitoa wito wa kufanyika kwa maandamano mapya leo Jumatano na Jumamosi kwa lengo la kushinikiza jeshi, linaloendelea kumtii rais aliyechaguliwa Nicolas Maduro, na kuunga mkono onyo la Ulaya kwa ajili ya uchaguzi huru.

"Jumatano kuanzia saa sita hadi saa nane mchana, nchini kote Venezuela tutamiminika mitaani (...) kuomba jeshi la nchi kuunga mkono madai ya wananachi, na Jumamosi (tunatoa wito) wa kufayika kwa maandamano kubwa nchini Venezuela na kwingineko duniani kuunga mkono onyo la Umoja wa Ulaya, "alisema Juan Guaido, Spika wa bunge la venezuela, mwenye umri wa miaka 35.

Siku ya Jumamosi nchi sita za Ulaya (Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ureno, Uholanzi) zilimpa Nicolas Maduro muda wa siku nane kuitisha uchaguzi, la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela. Muda huo utatamatika siku ya Jumapili.

Tayari Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini zimetangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.