Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Trump: Mchapishaji wa kitabu chenye utata alikiuaka sheria za uchapishaji

Rais wa Marekani Donald Trump anajaribu kuzuia kuchapishwa kwa kitabu chenye utata, ambapo baadhi ya mambo muhimu ya kitabu hicho tayari yametolewa katika vyombo vya habari na kitabu hicho kinatazamiwa kuwekwa sokoni leo Ijumaa badala ya Jumanne ya wiki ijayo.

Mshauri wa zamani wa Donald Trump, Steve Bannon, hapa ilikua mnamo mwezi Februari 2017 katika mkutano na Donald Trump (upande wa kulia) katika White House.
Mshauri wa zamani wa Donald Trump, Steve Bannon, hapa ilikua mnamo mwezi Februari 2017 katika mkutano na Donald Trump (upande wa kulia) katika White House. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Maoni ya mambo yanayomhusu rais Trump na familia yake yaliyozungumzwa ndani ya kitabu hicho, yametolewa na aliyekuwa msaidizi wa Trump Steve Bannon, zikiwemo tuhuma za familia ya Trump kukutana na watu kutoka Urusi ili kuingilia masuala ya uchaguzi wa Marekani ya mwaka 2017.

Rais wa Marekani alitaka kitabu hiki kuzuiliwa kuchapishwa, ambako anaelezewa kuwa "alitumiwa " na familia yake, huku Steve Bannon, mshauri wake wa zamani, akishutumu Donald Trump Jr, mwanae Donald Trump kufanya uhaini kuhusu suala la mkutano na maafisa wa Urusi mnano mwezi Juni 2016.

Mchapishaji wa kitabu chenye utata kuhusiana na rais Donald Trump amesema kuwa amevikabili vikwazo kutoka kwa wanasheria wa Trump wanaojaribu kuzuia kisichapishwe.

Kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la Fire and Fury kilichoandikwa na Michael Wolff kutokana na upinzani mkali wa uchapishwaji wake kwa sasa kinatolewa siku nne kabla ya muda uliotarajiwa.

Siku ya Alhamisi wanasheria wa Donald Trump waliomba kitabu hicho kisichapishwi, na kutishia kumfungulia mashitaka mchapishaji wa kitabu hicho. Wanasheria wa Trump wanachukulia kuhusu maelezo ya kitabu hicho, ambapo Michael Wolff anakubali kwamba "mengi ya habari kuhusu kile kilichotokea katika ikulu ya White House zinatafautiana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.