Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani: Seneti yapitisha muswada wa mabadiliko ya Kodi

Bunge la Seneti nchini Marekani limepitisha mabadiliko makubwa ya mfumo wa kodi, hatua ambayo sasa inaelekea kumpa ushindi wake wa kwanza mkubwa rais Donald Trump, mwaka mmoja baada ya kuchukua ofisi.

Spika wa bunge la wawakilishi, Paul Ryan kutoka chama cha Republican
Spika wa bunge la wawakilishi, Paul Ryan kutoka chama cha Republican REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa Republican wamepitisha muswada huo kwa misingi ya idadi ambapo wabunge 51 kati ya 48 wa Democrats waliunga mkono mabadiliko haya.

Wakati wa kura hii wabunge wote wa Democrats waliungana kupinga muswada wa mabadiliko haya.

Bunge la wawakilishi lilipitisha muswada huo bila kupingwa usiku wa kuamia leo huku kura ikitarajiwa kuwa ngumu kwenye bunge la Seneti.

Hata hivyo kiongozi wa walio wachache kutoka chama cha Democrats kwenye bunge la wawakilishi Nancy Pelos amekashifu mabadiliko yanayoenda kufanywa.

Kiongozi wa wachache katike bunge la wawakilishi nchini Merakani kutoka chama cha Democrats, Nancy Pelos.
Kiongozi wa wachache katike bunge la wawakilishi nchini Merakani kutoka chama cha Democrats, Nancy Pelos. REUTERS/Aaron P. Bernstein

Kwa upande wake spika wa bunge la wawakilishi kutoka cha cha Republican Paul Ryan amesema mabadiliko haya ni muhimu na Wamarekani watarajie kufanya karamu.

Hata hivyo wakosoaji wa mabadiliko haya ya kodi wanasema yatawanufaisha watu matajiri zaidi kuliko watu wa kati.

Kwa miezi kadhaa sasa wabunge wa kambi mbili wale wa Republican na Democrats wamekuwa wakivutana kuhusu kupitishwa kwa mabadiliko haya ambayo Rebublicans wanasisitiza yatakuwa na tija kwa taifa lao huku wapinzani wao wakidai yatawanufaisha matajiri pekee.

Rais Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii akiwapongeza wabunge wake katika bunge la wawakilishi ambao kwa kauli moja walipitisha muswada huu.

Saa chache kabla ya muswada huu kupitishwa kwenye usiku wa kuamkia leo kwenye bunge la wawakilishi kwa kuidhinisha dola Trilioni 1.5 za mabadiliko ya kodi, bado muswada huu utalazimika tena kurudi kwao baada ya kuondolewa kwa vipengele vitatu ambavyo vilidaiwa kwenda kinyume na sheria za bunge la Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.