Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Kimbunga Nate chapunguza kasi kwenye anga ya Mississippi na Alabama

Kimbunga hatari cha Nate kimegeuka kuwa kimbunga cha kitropiki siku ya Jumapili katika anga ya Alabama kusini mwa Marekani baada ya kupiga eneo hilo karibu na Mississippi ambakokilisababisha mafuriko na kuharibu barabara na majengo kadhaa.

Kimbunga Irma kilisababisha mafuriko katika miji kadhaa ya Marekani. Hapa ni katika mji wa Naples,Septemba 11, 2017.
Kimbunga Irma kilisababisha mafuriko katika miji kadhaa ya Marekani. Hapa ni katika mji wa Naples,Septemba 11, 2017. REUTERS/Stephen Yang
Matangazo ya kibiashara

Kimbunga Nate chenye upepo unaokwenda karibu kilomita 55 kwa saa kinaendelea kuelekea kaskazini mashariki.

Kituo cha vimbunga cha Marekani (NHC) kimeinua tahadhari zake kwa eneo hilo siku ya Jumapili asubuhi.

Kimbunga Nate ni kimbunga hatari cha nne kukumba Marekani ndani ya iipindi cha miezi miwili, baada ya Harvey, Irma na Maria, lakini kwa saa kimepoteza nguvu.

Kimbunga Nate kilipiga eneo la Marekani Kusini usiku wa Jumamosi karibu na Mississippi kisha Jumapili asubuhi katika mji wa Biloxi kusini mwa Mississippi, ambapo wakazi 46,000 walionywa dhidi ya hatari za mawimbi ya chini.

Barabara kadhaa ziliharibiwa kutokana na mafuriko maeneo mengine muhimu.

Siku ya Jumapili, viongozi wamekua wakionekana kufurahishwa na jinsi uharibifu ulikua katika kiwango kidogo.

"Sisi tuna bahati sana, asubuhi hii tumebarikiwa," alisema Gavana wa Mississippi Phil Bryant, akikumbusha kwambakimbunga Nate hakijasababisha maafa yoyote.

Kuwasili kwa kimbunga Nate pia kumesababisha mamlaka kusimamisha shughuli za bandarini. Uzalishaji wa mafuta na gesi pia umepungua.

Kabla ya kupiga Marekani, Kimbunga Nate kilipiga rasi ya Mexico ya Yucatan, inayojulikana kwa maeneo ya kitalii ya Cancun na Playa del Carmen. Siku ya Alhamisi, watu 16 waliangamia nchini Nicaragua, kumi nchini Costa Rica, wawili nchini Honduras na wawili nchini El Salvador.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.