Pata taarifa kuu
HAITI-CARABBEAN-TABIA NCHI

Hali ya tahadhari yatangazwa katika visiwa vya Saint-Barthélémy na Saint-Martin

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba uharibifu utakua mkubwa katika visiwa vinavyomilikiwa na Ufaransa katika eneo la Caribbean kufuatia kimbunga Irma, ambacho kimeelezwa kuwa "hatari sana" na Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Ufaransa.

Mafuriko yashuhudiwa katika bandari ya kisiwa cha Saint-Martinbaada ya kimbunga Irma kupiga eneo hilo, Septemba 6, 2017.
Mafuriko yashuhudiwa katika bandari ya kisiwa cha Saint-Martinbaada ya kimbunga Irma kupiga eneo hilo, Septemba 6, 2017. RCI GUADELOUPE/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Watu saba wamepoteza maisha huku mali ya watu kama nyumba zikiharibiwa kutokana na kimbunga Irma.

Rais Macron hakutoa maelezo zaidi kuhusu uharibifu huo.

Siku ya Jumatano, kimbunga Irma kilisababisha uharibifu mkubwa katika kisiwa cha Barbuda kabla ya kuelekea katika visiwavinavyo,ilikiwa na Ufaransa vya Saint-Barthélémy na Saint-Martin, ambavyo vimewekwa katika katika hali ya tahadhari, na marufuku kwa watu kutoka nje.

Maafisa wanahofia kuwa huenda, idiidi ya vifo ikaongezeka.

Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya visiwa hivyo, Anik Girardin amezungumzia janga hili kuwa ni baya kuwahi kutokea katika visiwa hivyo.

Jitihada za uokoaji zinatatizwa kutokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maene mengine.

Wakati huo huo upepo umetajwa kupata nguvu na kuwa vimbunga viwili.

Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.

Une photo satellite de l'ouragan Irma datée du 5 septembre 2017 et d'intensité maximale (catégorie 5 selon la météo américaine). Une photo prise par  l'Agence américaine d'observation océanique et atmosphérique.
Une photo satellite de l'ouragan Irma datée du 5 septembre 2017 et d'intensité maximale (catégorie 5 selon la météo américaine). Une photo prise par l'Agence américaine d'observation océanique et atmosphérique. NOAA vie Reuters

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.