Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-HAKI

Donald Trump amtimua Mkurugenzi wa FBI

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI James Comey alifutwa kazi na rais Donald Trump siku ya Jumanne Mei 9. Katika ujumbe mfupi, Ikulu ya White House ilisema kuwa kuondoka kwa James Comey "kutaruhusu shirika hilo kuwa na mwanzo mpya."

Aliye kuwa Mkuu wa FBI, James Comey, Aprili 26, 2016  Washington.
Aliye kuwa Mkuu wa FBI, James Comey, Aprili 26, 2016 Washington. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump amesema kuwa kufukuzwa kwa James Comey kumetokana na mapendekezo ya Waziri wa Sheria Jeff Sessions, ambaye anamshtumu James Comey kutowajibika vilivyo katika uchunguzi wa barua pepe za Hillary Clinton.

Bwana Sessions alisema kuwa Wizara ya Sheria ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, White haouse imesema.

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.