Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP

Aliyekuwa mshauri wa usalama wa Trump ataka kulindwa ili atoe ushahidi

Aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais wa Marekani Donald Trump ambaye alifutwa kazi, ameeleza kuwa anataka kupewa hakikisho la kutoshtakiwa ili atoe ushahidi wake mbele ya kamati inayochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa nchi hiyo.

Aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama kwa rais Trump,  Michael Flynn ambaye sasa ametaka kulindwa kabla ya kuzungumza.
Aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama kwa rais Trump, Michael Flynn ambaye sasa ametaka kulindwa kabla ya kuzungumza. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Mawakili wa Michael Flynn wanasema mteja wao anayo mambo ya kusimulia lakini anataka kulindwa dhidi ya hukumu ambayo haitakuwa ya haki.

Baraza la Seneti limeanzisha uchunguzi wake kuhusiana na tuhuma hizi, ambapo limeonya kuwa Propaganda za Urusi zilikuwa ni kama kimondo.

Flynn alifutwa kazi mwezi Februari baada ya kubainika kuwa aliidanganya ikulu kuhusu mawasiliano yake balozi wa Urusi.

Uhusiano wake na maofisa wa Urusi yamekuwa yanamulikwa na shirika la upelelezi FBI na kamati ya intelijensia ya Seneti.

Michael Flynn  wakati akiwasili kuonana na rais Trump kabla ya uteuzi wake na kisha baadae kufutwa kazi.
Michael Flynn wakati akiwasili kuonana na rais Trump kabla ya uteuzi wake na kisha baadae kufutwa kazi. ©REUTERS/Mike Segar

“Jenerali Flynn anayo mambo ya kusimulia, na yuko tayari kueleza, ikiwa hali itaruhusu,” amesema mwanasheria Robert Kelner.

Flynn amesema kuwa hatatoa maoni yoyote kuhusu majadiliano yake na baraza la Congress ambalo na lenyewe linachunguza tuhuma hizi kuwa Moscow ilimsaidia rais Trump kuingia madarakani.

Hata hivyo wakili wa Flynn alikataa kuweka wazi ikiwa mteja wake alikuwa anataka apewe hakikisho la kulindwa ikiwa atazungumza.

Uchunguzi wa baraza la seneti umefunguliwa Alhamisi ya wiki hii, huku mwenyekiti wake Mark Warner akisema kuwa Urusi ilipora uchaguzi wa mwaka jana kwa lengo la kumsaidia Trump kushinda.

Warner ambaye ni mbunge wa chama cha Democrats anasema Urusi inaweza kuwa ilitumia teknolojia yake kusambaza taarifa za uongo kwa wapiga kura kwenye baadhi ya majimbo kama ya Wisconsin, Michigan na Pennsylvania.

Mbunge mmoja wa Republican Richard Burr amesema kila mmoja wao alilengwa na teknolojia adimu ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.