Pata taarifa kuu
GUATEMALA-AJALI

Wasichana 31 waangamia katika ajali ya moto Guatemala

Wanaharakati wengi wa haki za binadamu wameandamana Alhamisi wiki hii mbele ya Ikulu ya rais wa Guatemala baada ya wasichana 31 kupoteza maisha Jumatano jioni kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika kituo kinachowalea watoto katika eneo la San Jose Pinula.

Wanaharakati wngi wa haki za binadamu wameonyesha hasira baada yatukio la ajali ya moto.
Wanaharakati wngi wa haki za binadamu wameonyesha hasira baada yatukio la ajali ya moto. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Guatemala Jimmy Morales alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na kumfuta kazi Mkurugenzi wa kituo hicho.

Unyanyasaji wa kijinsia na lishe duni

Baadhi ya wasichana walionusurika wameandamana dhidi ya lishe duni na unyanyasaji wa kijinsia ambapo wanasema kuwa waliathirika Jumanne usiku na Jumatano kabla ya ajali moto kutokea.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashitaka inayohusika na Haki za Binadamu ikinukuliwa na shirika la habari la AFP, moto huo ulisababishwa na waathirika wenyewe kwa kushtumu vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia wanavyofanyiwa na maafisa wa kituo hicho.

Kituo hiki kilifunguliwa mwaka 2006 kwa ajili ya kuwapokea watoto na vijana waathirika wa vurugu za familia na watoto wa mitaani, kituo hiki kina uwezo wa kuwapokea watoto 400.

Lakini vyombo vya habari vya Guatemala vinabaini kwamba kituo hiki kina uwezo wa kupokea watoto 800.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.