Pata taarifa kuu
GUATEMALA-UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Guatemala wapiga kura katika hali ya utulivu

Raia nchini Guatemala wameshiriki uchaguzi Jumapili mwishoni mwa juma hili, baada ya rais wa nchi hiyo kukamatwa kwa tuhuma za rushwa na kuwekwa kizuizini kwa muda, huku makamu wa rais akiapishwa kuwa rais.

Mwanamke huyu akipiga kura katika kituo cha kupigia kuracha San Pedro Sacatepéquez, nje kidogo ya mji wa Guatemala, Septemba 6, 2015.
Mwanamke huyu akipiga kura katika kituo cha kupigia kuracha San Pedro Sacatepéquez, nje kidogo ya mji wa Guatemala, Septemba 6, 2015. REUTERS/Josue Decavele
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu milioni 7.5 wa Guatemala wamepiga kura Jumapili Septemba 6 kumchagua rais wao mpya, wabunge pamoja na wakuu wa majimbo. Uchaguzi umefanyika katika hali isiyoeleweka kufuatia rushwa ambayo imekithiri nchini humo, baada ya wiki ya kihistoria ambapo kulishuhudiwa Rais Otto Perez, akituhumiwa kuendesha mtandao wa rushwa katika ya Idara ya Forodha, na baadae kupoteza kinga yake, kujiuzulu na kisha kuwekwa chini ya ulinzi hadi Jumanne Septemba 1.

Cha kushangaza, ni kuwa uchaguzi umeanza katika hali ya utulivu. hata hivyo kumeshuhudiwa katika mikoa mbalimbali barabara nyingi zikifungwa na makundi ya watu wakitafuta kuzuia wapiga kura waliokuwa wakisafirishwa na vyama vyao vya siasa kwenda kupiga kura. Polisi iliingilia kati mara kadhaa ili kurejesha hali ya kawaida barabarani au kutatua migogoro ambayo imesababisha mapigano kati ya wapiga kura.

Aidha, hata kabla ya ufunguzi wa baadhi vituo vya kupigia kura, kulionekana watu wengi wakipanga foleni ya kwenda kutumbukiza kura zao katika sanduku za kura. Lakini haijulikani iwapo raia wengi wamefanikiwa kupiga kura.

Masaa kadhaa baada ya kuanza kwa upigaji kura, Mahakama kuu ya Uchaguzi imekitaja kitendo hicho kuwa hakikubaliki, huku ikiwa na imani kuwa idadi ya wapiga kura itaongezeka. Tena ni kujua kama kweli hali hii itaendelea, kwa sababu uchaguzi huu umefanyika katika mazingira ya mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na rushwa, na katika hali hii, raia wa Guatemala wamegawanyika kwa siku ya Jumapili hii. Baadhi wanaunga mkono mchakato wa uchaguzi na wamekwenda kupiga kura, huku wengine wakitolea wito kwa wapiga kura kususia uchaguzi huo au kufuta kura zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.