Pata taarifa kuu
MAREKANI-GUANTANAMO-UGAIDI

Marekani: Obama mbioni kuifunga jela ya Guantanamo

Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali yake itawasilisha mbele ya Baraza la Wawakilishi mpango wa kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay. Kufungwa kwa jela hiyo ni moja ya malengo ya Rais wa Marekani Barack Obama ambayo alikua mpaka sasa bado hajatimiza.

Jela ya Guantanamo Bay.
Jela ya Guantanamo Bay. AFP/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House imesema kwamba mpango huo utawasilishwa Jumanne hii na Pentagon mbele ya Baraza la Wawakilishi.

Rais Barack Obama amesema anataka kufunga gereza hilo kabla ya kuondoka madarakani mapema 2017.

Wizara ya ulinzi ya Marekani imependekeza wafungwa 91 ambao bado wanazuiliwa katika gereza hilo warejeshwe katika nchi zao au wahamishiwe katika magereza ya jeshi la Marekani au katika magereza ya kiraia.

Hata hivyo Baraza la Wawakilishi limekuwa likipinga wazo hilo na linatarajiwa kupinga mpango huo wa Rais Obama.

Maafisa wakuu wa utawala wa Obama wamewambia waandishi wa habari Jumanne kwamba kufungwa kwa jela hiyo ni kwa maslahi ya usalama wa kitaifa.

"Kutekelezwa kwa mpango huu kutaimarisha usalama wa taifa kwa kuwanyima magaidi nguvu muhimu ambayo wamekuwa wakitumia katika harakati zao, kuimarisha uhusiano na marafiki wakuu na washirika katika kukabiliana na ugaidi,” afisa wa vyombo vya habari wa Pentagon Peter Cook amesema.

Jela ya Guantanamo inmesalia na wafungwa 105 pekee, lakini watu 780 walizuiliwa katika jela hiyo tangu mwaka 2002. Hata hivyo wafungwa hamsini wamo mbioni kuachiwa huru, baada ya kuidhinishwa.

Maandamano ya shirika la kimataifa ya hakiza binadamu la Amnesty International mbele ya Ikulu ya White House , Januari 16, 2016, kwa kufunga jela ya Guantanamo Bay.
Maandamano ya shirika la kimataifa ya hakiza binadamu la Amnesty International mbele ya Ikulu ya White House , Januari 16, 2016, kwa kufunga jela ya Guantanamo Bay. REUTERS/Jonathan Ernst

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.